Posted by Esta Malibiche on Oct 28.2016 in KITAIFA
Mkuu
wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza baraza la
wafanyakazi mkoani humo katika kipindi cha mwaka 2016/2019(picha na
Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU wa mkoa wa
Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka maafisa utumishi kuwapa
nafasi baadhi ya wafanyakazi wanaoomba kwenda kujiendeleza kitaaluma
badala ya kuwabania na kusababisha kudumaa kielimu.
Aidha ametoa
rai kwa watumishi wa umma mkoani humo kuwajibika kwenye maeneo yao ya
kazi pamoja na kuwatumikia wananchi kikamilifu.
Mbali na hayo
mkuu huyo wa mkoa ,amesisitiza viongozi mbalimbali kwenye maeneo ya
kazi kujenga ushirikiano wa kutosha na wafanyakazi /watumishi ili
kuondoa malalamiko ambayo huwa yakijitokeza .
Mhandisi
Ndikilo aliyasema hayo ,wakati akifungua baraza la wafanyakazi mkoani
Pwani mwaka 2016-2019 pamoja na kuchagua katibu na katibu msaidizi wa
baraza hilo.
Hata hivyo
alisema ni lazima kukubaliana na mabadiliko na kwenda na wakati kwa
kukuza taaluma za watumishi ili kuongeza uwezo kwenye maeneo yao ya
kazi .
"Kiukweli
tuliyojifunza darasani isiwe mwisho badala yake tuongeze elimu zetu kwa
lengo la kupanua elimu zetu ambazo wengi wetu tumezipata miaka mingi
iliyopita" alisema.
Mhandisi
Ndikilo, alieleza kuwa ifikie wakati wa kujitambua na kuthamini nafasi
walizonazo na kutamani kufika kwenye hatua nzuri ya kielimu.
Akizungumzia
suala la uwajibikaji aliwaomba maafisa utumishi na makatibu tawala
wilaya na mkoa waendelee kuwa wawakilishi wakubwa wa kuwasilisha kero
zinazowakabili watumishi .
Alisema uwajibikaji kazini ni nguzo pekee ya ufanisi kazi hivyo kuna kila sababu ya viongozi kuwa na ushirikiano na watumishi .
"Wote tupo
sawa na kila mmoja anafanyakazi kwenye nafasi yake ,hakuna mkubwa
zidi ya mwenzie kwa kumfanya mwengine amsujudie hadi kuogopana
kazini.
" Kikubwa ni
kuheshimiana ,kuwa na upendo na kuthaminiana bila kudharauliana ama
kutokana na nafasi yako ya juu ndio ukandamize wengine.alisisitiza.
Nae afisa
kutoka ofisi ya waziri mkuu ,kazi,ajira,vijana na wenye ulemavu
,Honesta Ngolly aliyataka mabaraza ya wafanyakazi yatumie meno yake
kusimamia kero za wafanyakazi.
Alisema watumishi wana haki ya kujiendeleza kielimu na hakuna serikali ambayo imekataza watumishi kujiendeleza.
Honesta alisema endapo watumishi watakuwa wakiongeza elimu zao itawezesha kuongeza ufanisi makazini.
Mwenyekiti wa
baraza la wafanyakazi mkoani Pwani Edward Mwakipesile alisema mawazo na
maagizo waliyopewa watayafanyia kazi ili kulinda maslahi na haki za
watumishi.
Mwakipesile
aliomba ushirikiano na uwajibikaji uendelee katika mkoa huo ili kupiga
hatua kutoka mkoa ulipo na kuwatumikia wananchi .
Awali kabla ya
kufunguliwa baraza hilo Pascal Dawson alichaguliwa kuwa katibu wa
baraza la wafanyakazi mkoani hapo na katibu msaidizi Asha Itelewe.
Mwisho
0 maoni:
Chapisha Maoni