Alhamisi, 13 Oktoba 2016

NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI SULEIMAN JAFO AWAAGIZA WAHANDISI WA MAJI KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI

Posted by Esta Malibiche on Oct13.2016 in NEWS

jf1
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akiwa katika Ukaguzi wa ujenzi wa Lambo la kuvuna maji ya mvua wilayani kilindi



Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo,  amefanya ziara katika Halmashauri 6 za mikoa ya Tanga na Manyara huku akiwaagiza Wahandisi wa maji wa Halmashauri hizo kusimamia vyema miradi ya maji inayoendelea kujengwa katika halmashauri hizo.
Halmashauri alizofanya ziara yake ni pamoja na halmashauri ya wilaya ya kilindi Kiteto, Babati Mji, Babati, Mji Mbulu na Halmashauri ya Mbulu vijijini.
Katika ziara hiyo pia alifanikiwa kuzungumza na watumishi na kutembelea miradi ya Elimu, Afya, Maji na Miundombinu ya barabara.
Akizungumza na watumishi, Jafo aliwaagiza wahandisi wa maji kusimama imara katika kusimamia miradi ya maji inayo endelea kujengwa ili miradi hiyo iweze kuwa na ubora unaokusudiwa ili kuondoa changamoto za upatikanaji wa maji katika jamii.
“Kila mradi wa Maji lazima uwe chini ya usimamizi wa chombo cha watumia maji ili miradi hii iwe endelevu,”amesema Jafo
jf2
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akikagua ujenzi wa barabara za halmashauri na ujenzi wa madaraja Katika halmashauri ya wilaya ya kilindi
jf3
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi)akisaini kitabu cha wageni alipokuwa akikagua hospitali ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
jf4

0 maoni:

Chapisha Maoni