Posted by Esta Malibiche on Oct8.2016 in NEWS
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amekutana na wajumbe wa baraza la ardhi la wilaya hiyo na kupanga mikakati ya kutatua migogoro katika kata mbalimbali.
Akizungumza
na Waandishi wa habari ofisini kwake jana Mjema alisema kuwa kuanzia
sasa ataanza kuzunguka na wajumbe hao wa baraza katika kata mbalimbali
ili waweze kujionea kwa macho tatizo la migogoro ya ardhi linalo
wakabili.
“Hiki ni kikao cha kawaida tu chenye lengo la kupanga mipango mbalimbali
ya kutatua changamoto zinazo wakabili wakazi wa Ilala haswa Migogoro ya
ardhi” anasema Dc Sophia Mjema
Alisema lengo la ziara ni pamoja na kujenga mshikamano wa kikazi baina
ya wananchi na Watendaji wa Serikali katika kutatua kero zao.
Ilala Dar es salaam,Tanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni