Posted by Esta Malibiche on Oct 28.2016 in NEWS
Na Fatma Kassim
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod
Thabit Kombo amesema kuwa na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ina
nafasi kubwa ya kufanya uchunguzi ambao unasaidia kutatua matatizo
mbalimbali kiafya katika jamii.
Amesema kutokana na kuwa Bodi
hiyo inawalinda wananchi na mambo mbalimbali yanapelekea madhara ni
vyema kufanya kazi kwa uwadilifu na kuishauri Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali kufanya kazi kwa jitihada zote ili kuepusha matatizo ya kiafya
kwa jamii.
Akizindua Bodi ya Ushauri ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Waziri wa Afya ameitaka bodi hiyo
kuandaa mipango madhubuti itakayosaidia kuondosha mapungufu
inayowakabili Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Amesema kutokana na kuwa maabara
hiyo inafanya uchunguzi wa mambo mbalimbali ikiwemo vyakula,vinywaji na
dawa za binaadamu pamoja na kudhibiti kemikali zinatumiwa viwandani na
majumbani hivyo amewataka kufanya kazi kwa mashirikiano na taasisi
mbalimbali ikiwemo bodi ya chakula dawa na vipodozi na shirika la
viwango
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi
hiyo Dk Yussuf Nuhu Pandu amesema watahakikisha wanafakazi kwa mujibu
wa sheria zilizowekwa ili kuweza kufanikisha maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali kufanyakazi zake kwa uadilifu.
Amesema kutokana na kazi za
Maabara ni kulinda afya za Wazanzibar pamoja na mazingira yao kwa
kuchunguza ubora wa chakula na kemikali watafanya kila jitihada kuona
mambo hayo yanafanyika .
Nae Mkemia Mkuu wa Maabara ya
Serikali Dk Slim Rashid Juma amesema wameweza kupata mafanikio
mbalimbali ikiwemo kuwa na sheria ya maabara namba 10 ya mwaka 2011
inayoipa maabara hadhi ya wakala wa Serikali.
Mafanikio mengine ni Serikali
kuwapatia majengo matatu katika eneo la Maruhubi Unguja na jengo
jengine eneo la Madungu Pemba kwa matumizi ya maabara
Amesema licha ya mafanikio hayo
pia wanakabiliwa na changamoto na uchakavu na uchache wa vifaa na
mashine za kufanyia uchunguzi pamoja na uchache wa kemikali ambalo
linashusha utendaji wa kazi za maabara.
0 maoni:
Chapisha Maoni