Posted by Esta Malibiche on Oct 29.2016 in MICHEZO
Akimkabidhi,Siza Hans Pope akimkabidhi vifaa vya Michezo Mratibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Iringa,Kennedy komba kwa
niaba ya
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa timu ya Simba Hans Pope.
Siza Hans Pope akimkabidhi vifaa vya Michezo Mratibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Iringa,Kennedy komba kwa
niaba ya Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa timu ya Simba Hans PopeJezi seti nne zilizotolewa na mdau wa Michezo Nchini Hans Pope kwa Jeshi la Zima moto
Siza Hans Pope akizungumza na kikosi cha jeshi la Zimamoto mara baada ya kukabidhi vifaa vya Michezo
Picha zote na Esta Malibiche[KALI YA HABARI BLOG]
Na Esta Malibiche
Iringa
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa
timu ya Simba Hans Pope amekabidhi vifaa vya Michezo vyenye thamani ya
Mill.2,900000 kwa kikosi cha timu ya Jeshi la Zima moto Mkoani Iringa
Akimkabidhi Mratibu wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Iringa, kwa niaba ya Hans Popo,Siza Hans alisema
kuwa ameamua kuisaidia timu hiyo vifaa vya michezo ili iweze kucheza kwa bidii na hatimae timu iweze
kusonga mbele.
“Sote tunatambua umuhumu wa michezo katika jamii,hivyo tumeona
tutoe msaada huu ili uisaidia timu ya zimamoto kujiweka fiti katika suala zima
la afya, kiakili. Tunajua ugumu na shida ambazo zinakaibili timu nyingi za soka
na michezo mingine mbalimbali hapa Nchini ninawaomba na wadau wengine waendelee
kujitolea ili kutatua changamoto hizo’’’’’’’alisema Sinza
Aidha aliitaka Serikali kurudisha
michezo katika Shule za Msingi na
Sekondari ili wananfunzi mara
wamalizapo waweze kuendelea kuipenda michezo
na hatimae kuwa wachezaji wazuri hapo baadae.
‘’’Kitendo cha serikali kuondoa michezo
katika shule za msingi
na sekondari Nchini ndiyo chanzo kikubwa cha kuyumba kwa michezo mbalimbali nchini Tanzania. Endapo Serikali itarejesha michezo shuleni ,kutakuwa na Mwamko mkubwa wa michezo na hatimae vipaji vingi vitaibuka.’’’’’alisema
na sekondari Nchini ndiyo chanzo kikubwa cha kuyumba kwa michezo mbalimbali nchini Tanzania. Endapo Serikali itarejesha michezo shuleni ,kutakuwa na Mwamko mkubwa wa michezo na hatimae vipaji vingi vitaibuka.’’’’’alisema
Aliongeza kuwa wakati michezo ilipokuwa ikifundishwa
katika shule za msingi na sekondari mwamko
wa kuipenda michezo ulikuwa mkubwa kwa kila mwananchi na kiwango
cha michezo kilionekana tofauti na hivi sasa .
cha michezo kilionekana tofauti na hivi sasa .
Kwa upande wake Mratibu wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Iringa,kamanda KennedyKomba, akimshukuru Zakaria
Hans Popokwa msaada wa seti nne za jezi na soksi nakusema kuwa msaada huo,alisema
kuwa vifaa hivyo vimekuja kwa wakati muafaka kutokana na kikosi hicho kuwa
katika mazoezi makali ya kujiandaa na mashindano yanayotarajia yatakayfanyika Mkoani hapa hivi karibuni.
katika mazoezi makali ya kujiandaa na mashindano yanayotarajia yatakayfanyika Mkoani hapa hivi karibuni.
Komba alisema hapo awali timu
hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya Michezo,hivyo msaada huo umewapa
moyo na nguvu na kuwafanya waone kuwa jamii inakitambua kikosi cha zimamoto katika suala la kukuza michezo kwa kikosihicho.
moyo na nguvu na kuwafanya waone kuwa jamii inakitambua kikosi cha zimamoto katika suala la kukuza michezo kwa kikosihicho.
Hilaly Kobelo ni Mkaguzi Msaidizi wa
Zimamoto mkoa wa Iringa,ambae pia ni nahodhawa wa kikosi cha Timu hiyo alisema kuwa, kikosi hicho
kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wavifaa vya michezo hivyo msaada
huo utawasaidia katika kujiandaa na michezombalimbali.
Kobelo alisema mikakati ya kuanza kuipandisha daraja timu
hiyo hadi kufikiangazi ya ligi kuu imeanza, na hii itawasaidia hata kupata
wadhamini endapo timu hiyo itafanya vizuri katika mashindano yajayo watakayoshiriki
MWISHO
0 maoni:
Chapisha Maoni