Posted byb EstaMalibiche on Oct18.2016 in NEWS
Mkuu
wa kitengo watu wenye tatizo la ugonjwa wa Usonji (National Association
for People with Autism –Head) Dkt Stella Rwezaula (kulia) akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kuzindua warsha maalum kwaajili ya kuoa
uelewa kwa watu mbalimbali kuhusu tatizo la Usonji nchini, anaefuata ni
Dialla Kassam ambaye ni kurugenzi wa kituo cha Afya cha LOTUS ambao
ndio wazamini wa warsha hiyo, akifuatiwa na mtaalam wa mambo ya usonji
dunia bw, Kevin Baskerville, kutoka Leicestershire, UK, pamoja na Meneja
wa kituo cha Lotus Bi Deepack Gorecha kushoto.
Wapili toka kushoto ni Mtaalam wa mambo ya Usonji toka UK bw, Kevin Baskervile
akikabidhi mfumo maalum alioubuni kwaajili ya kusaidia kufundisha
watoto wenye usonji kwa dokta Stela Rwezaula toka muhimbili ili kusaidia
kufundisha watoto wanaopatwa na tatizo hilo kupata elimu kwa njia ya
picha. katikati anaeshuhudia
ni mkurugenzi wa kituo cha afya kinachosaidia watoto wenye usonji Bi Dialla Kassam na Deepak Gorecha (kushoto) wakishuhudia. Aliyesimama ni Mtaalam wa tatizo la Usonji toka UK bw Kevin Baskervile toka UK akitoa mada kwa wadau mbalimbli wakati wa warsha maalum kwaajili ya kueneza uelewa kuhusiana na tatizo
la usonji nchini.

Wapili
toka kulia ni mkuu wa kituo cha afya kinachosaidia wagonjwa wa Usonji
nchini Bi Dialla Kassam akiongea na waandishi wa habari kuhusu udhamini
wao wa warsha maalum ya kuongeza uelewa wa usonji kwa wadau mbalimbali
nchini wakiwemo wazazi, anaefuata ni mtaalam wa tatizo la
usonji toka UK bw, Kevin Baskerville, Meneja wa kituo cha afya cha LOTUS bi Deepak Gorecha na Mkuu wa kitengo kinachoshughulikia watoto wenye usonji dkt Stella Rwezaula.
usonji toka UK bw, Kevin Baskerville, Meneja wa kituo cha afya cha LOTUS bi Deepak Gorecha na Mkuu wa kitengo kinachoshughulikia watoto wenye usonji dkt Stella Rwezaula.
-
Usonji bado changamoto kubwa Tanzania
Tanzania
bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na ugonjwa wa
usonji ambao wengi hawautibu kutokana na kutoelewa dalili zake,
imefahamika.
Hili lilielezwa na mkuu wa Chama Cha watu wenye Usonji Kitaifa (NAPA-T) Dr Stella Rwezaula katika mkutanona
waandishi wa habari.
waandishi wa habari.
“Dalili
za usonji bado hazijafaamika vizuri kwa wazazi na walimu nchini hivi
wanashindwa kuutibu ugonjwa huu au kupata msaada wa kitaalamu kwani ni
ugonjwa ambao una mambo mengi yanayoathiri namana mtu anavyowasiliana na
mara nyingi huwa na tabia ya kufanya vitu kwa kurudia rudia bila
kukusudia,” alisema.
Alisema
kwa mwaka huu, kituo cha Afya cha Lotus (LHC), ambacho sio cha serikali
na kinafanya kazi za kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu,
kimeifadhili NAPA-T kufanya warsha inayolenga kutoa elimu kuhusu usonji
na warsha hii itawaleta pamoja washiriki takriban 100 kutoka sekta
binafsi na za kiserikali. “Hu ni moja wa mkakati wa LHC kutoa elimu
katika jamii na kuwaleta pamoja watoto na wazazi wenye mahitaji
maalumu,” alisema.
Alisema
mojawapo wa kazi za NAPA-T kwa kushirikiana na LHC ni kutoa elimu na
mafunzo ya kutosha kuhusu ugonjwa huu ikiwemo katika serikali na mitaa
na serikali kuu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa LHC, Dialla Kassam, alisema wanajivunia kufanya kazi na
NAPA-T na kumshukuru mfadhili kutoka Uingereza, Kevin Baskerville,
ambaye ni mtaalamu wa ugonjwa huu wa usonji, kwa msaada wake kwani
amekuwa akija Tanzania mara kwa mara kutoa mafunzo na elimu kuhusu
usonji.
“Kupitia warsha iliyoandaliwa na LHC mwaka jana, International School of Tanzanyika (IST) ilishirikiana na
Shule ya Msimbazi Mseto ya watoto wenye mahitaji maalumu na watoto wa Msinbazi Mseto sasa wanaruhusiwa kwenda IST kuogelea matra moja kwa wiki,” alisema na kuongeza kuwa LHC inafaya kila jitihada kuunganisha shule zenye mahitaji maalumu na shule za serikali.

LHC pia imekuwa ikitoa msaada kwa shule ya watu wenye Usonji ya Mbuyuni
kwa kupitia wataalamu wa kujitolea kutoka pembe zote za dunia na
kusimamiwa na LHC ambayo pia hutoa rasilimali za elimu kwa shule
hiyo.
“Kwa
msaada wa Kevin, tumeweza kujenga ushirikaino wa muda mrefu na shule ya
watoto wenye mahitaji maalumu iliyoko uingereza iitwayo Hope School
iliyoko Newark ambayo imeahidi kuendelea kutoa msaada wa vifaa na
mafunzo kwa shule ya Msimbazi Mseto ambayo ni ya serikali,” alisema.
Alisema LHC pia inafanya kazi kwa karibu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hasa kitengo cha watu wenye
matatizo ya akili, ili kutafuta wafadhili ili kuanzisha kituo cha kwaza kabisa cha watu wenye mahitaji maalumu nchini. Kituo hicho kitakuwa na wataalamu wa kutosha ambao watakabiliana na matatizo mbalimbali ya kiakili ikiwemo usonji.

Baadhi ya dalili za usonji ni mtoto kutoweza kumtizama mtu machoni, kutoitika wakati anaitwa, kushindwa
kucheza na watoto wenzake wenye umri sawa, kushindwa kuwasiliana na wenzake, kukataa kubebwa na kukumbatiwa, kutamani kuwa peke yae muda wote na kushindwa kuonesha au kuelewa hisia mbalimbali.
kucheza na watoto wenzake wenye umri sawa, kushindwa kuwasiliana na wenzake, kukataa kubebwa na kukumbatiwa, kutamani kuwa peke yae muda wote na kushindwa kuonesha au kuelewa hisia mbalimbali.
Dalili nyingine ni tabia kubadilikabadilika, kuwa mgomvi, kutopenda mabadiliko, kuchelewa kuzungumza,
kurudiarudia mambo Fulani kama vile kutikisa kichwa, kuchezesha mikono, kunyatanyata na kuzungukazunguka.
kurudiarudia mambo Fulani kama vile kutikisa kichwa, kuchezesha mikono, kunyatanyata na kuzungukazunguka.
0 maoni:
Chapisha Maoni