Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amebainisha kuwa Serikali itaendelea kupambana kwa
hali na mali kuhakikisha wanapambana na tatizo la ugonjwa wa Saratani ya
Matiti hapa nchini ikiwemo kutoa elimu na tiba kwa Wananchi wake.
Hayo
ameyasema mapema leo Oktoba 29.2016 Jijini Dar es Salaam wakati wa
matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa saratani ya matiti
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Saratani ya Hospitali ya Ocean Road jijini
Dar es Salaam ambapo huu ni mwaka wa nne tokea yameanzishwa.
Ambapo
akihutubia wananchi mbalimbali pamoja na vikundi vya wataalamu na wadau
wa masuala ya mapambano ya Saratani hapa nchini, Dk.Kigwangalla amesema
kuwa jitihada mbalimbali zinafanywa na Serikali kwa kushirikiana na
wadau wengine ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.
“Kwa
hapa kwetu Tanzania wagonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi ni wengi
zaidi kuliko wagonjwa wa saratani ya matiti. Kila mwaka takribani ya
watu 44,000 wanapata saratani lakini hawafiki Hospitali kwa sababu
mbalimbali na ni asilimia 10 tu ya wagonjwa ndio wanaofika Hospitali kwa
uchunguzi na matibabu” alieleza Dk.Kigwangalla wakati wa kusoma hotuba
yake hiyo.
Hata
hivyo amewaondoa hofu wananchi juu ya dhana kuwa mtu haponi ugonjwa
huo jambo ambalo si kweli zadi ni ni elimu inahitajika zaidi pamoja na
tiba.
“Tuwe
na taratibu za kufanya uchunguzi wa mara kwa mara. Tuachane na dhana
potofu kama sratani haitibiki, Jitokeze kucheki tatizo na wataalam
watakupa huduma kukabiliana na ugonjwa huo. Kama tulivyoshuhudia baadhi
ya waliotoa shuhuda leo hapa” alimalizia Dk.Kigwangalla.
Awali
katika tukio hilo, Dk.Kigwangalla na wageni wengine mbalimbali waliweza
kufanya matembezi ya hisani ya zaidi ya KM 4. Yaliyoanzia katika viunga
hivyo vya Hospitali ya Ocean Road kasha kuzunguka katikati ya Jiji la
Dar es Salaam.
Fedha mbalimbali zilichangishwa katika tukio hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni