Posted by Esta Malibiche on Oct18.2016 in NEWS
Mwonekano wa Mv Nyehunge kwa ndani, sehemu ya abiria kukaa.
Na George Binagi
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, mwishoni mwa wiki amefanya uzinduzi
wa Meli Mpya ya Mv Nyehunge ya pili (II) inayofanya safari zake kati ya
Mwanza na Ukerewe na kuwataka wakazi wa Ukerewe kuitumia fursa hiyo
kujiinua kiuchumi.
Mongella
alisema Meli hiyo itasaidia kuondokana na adha ya usafiri kwa wakazi wa
Visiwa vya Ukerewe kwa kuwa imeongeza idadi ya Meli zinazofanya safari
kati ya Jiji la Mwanza na visiwa hivyo.
Aliwataka
wananchi kutumia fursa hiyo kusafirisha bidhaa zao kati ya Ukerewe na
Jiji la Mwanza ili kujiinua kiuchumi huku akisisitiza Kampuni ya
Nyehunge inayomiliki Meli hiyo kuzingatia vigezo vya usalama katika
uendeshaji wa safari zake.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyehunge, Said Mohame, alisema Meli hiyo
inaongeza safari kati ya Visiwa vya Ukerewe na Jiji la Mwanza na kufikia
safari tatu kwa siku huku suala la nauli nafuu likizingatiwa ili
kuondoa changamoto ya usafiri waliyokuwa nayo wakazi wa Ukerewe. Nauli
za Ukerewe katika Meli hiyo ni Shilingi 6,000 kwa 7,000.
Baadhi
ya wasafiri wa Ukerewe walipongeza ujio wa Meli ya Mv Nyehunge ambapo
wamebainisha kwamba itawasaidia kusafirisha kwa wakati bidhaa na mazao
ya chakula kati ya Ukerewe na Jiji la Mwanza.
Meli
hiyo ya Mv Nyehunge II ina uwezo wa kubeba abiria 500, magari madogo 40
na tani 284 za mizigo ambapo imejengwa na kampuni ya wazawa ya Songoro
Marine Transport ya Jijini Mwanza kwa zaidi ya shilingi Milioni 800.
0 maoni:
Chapisha Maoni