Posted by Esta Malibiche on Oct19.2016 in NEWS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akipata maelezo kutoka
kwa Bw. Mutagabaya Mtaalamu kutoka maabara maalumu ya kutunza Vyura ya
Kihansi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa
Kijiji cha Mwantasi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, aliposimama akiwa
katika ziara ya kikazi ya kukagua masuala ya mazingira.
Mjumbe wa Kamati ya Mazingira ya
Kijiji cha Mwantasi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa akipokea kiasi cha
Shilingi laki moja zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba kuchangia Mfuko wa
Mazingira wa Kijiji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na ujumbe wake
wakikagua mitambo ya kusukuma maji katika Mkoa wa Iringa, wa kwanza
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza.
…………………………………………………
Na Lulu Mussa
Kilolo – Iringa
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesisitiza
umuhimu wa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa shughuli zifanywazo na
binadamu kando ya Vyanzo hivyo hupelekea mito hiyo kukauka.
hayo yamebainishwa leo na Waziri
Makamba alipofanya ziara ya kikazi Kihansi Wilayani Kilolo kuangalia
chanzo cha Mto Kihansi. Waziri Makamba kwa nyakati tofauti amefanya
mazungumzo na wanakijiji wa Kijiji cha Mwantasi ambao wamefanya jitihada
za dhati kuhifadhi Vyanzo vya Maji.
Waziri Makamba amewapongea na
kuchangia kiasi cha shilingi laki mbili kwa vijiji vya Mwantasi kwa
ajili ya Mfuko wa Mazingira wa Kijiji wenye lengo la kusimamia masuala
za mazingira katika kijiji chao.
“Nawapongeza sana kwa jitihada
mlizonazo ikiwa ni pamoja na kuwa na sheria ndogo ndogo za kutunza
mazingira, nami nawaunga mkono kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki
moja kwa kijiji cha Mwantasi na laki moja kwa kijiji cha Wangama ili
kuimarisha mfuko huo” Makamba alisisitiza.
Aidha Waziri Makamba amemuagiza
Mkurugenzi wa Kilolo kuhakikisha fani zinazotozwa za uharibifu wa
mazingira sehemu ya pesa hizo zinapelekwa katika vijiji husika ili
kukuza mfuko huo na kuwaagiza wajumbe wa Kamati za Mazingira ngazi ya
kijiji kuzitunza fedha hizo benki na kuagiza matumizi sahihi.
Waziri Makamba anaendelea na
ziara ya kikazi katika Mikoa mbalimbali hapa nchini na leo yuko katika
Mkoa wa Morogoro ambapo ametembelea Mto Kihansi na Ruaha Mkuu.
0 maoni:
Chapisha Maoni