Posted by Esta Malibiche on Oct19.2016 in MICHEZO
Mbunge wa jimbo la kilolo
Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa
wanamichezo wa kijiji cha Bomalang’ombe wakati wa mkutano wa hadhara
ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji
cha Bomalang’ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo
la kilolo

ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya wanawake
wa kijiji cha Bomalang’ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na
mbunge wa jimbo la kilolo
Mbunge wa jimbo la kilolo
Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa
wanamichezo wa kijiji cha Bomalang’ombe wakati wa mkutano wa hadhara
ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji
cha Bomalang’ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo
la kilolo
………………………………………………………………………
Na Fredy Mgunda Iringa.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo
Vennance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi
kwa Vijana na timu za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya
wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.
Mwamoto ametekeleza ahadi hiyo
katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika
ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kwa
kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa vifaa
hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa
ni kutokana na ahadi yake yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao
kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa
hivyo ambapo sasa anafanya ili kutekeleza.
“Niliahidi kuleta vifaa vya
Michezo kwa kila Kata.Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahidi kuwaletea
vifaa na leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mwamoto.
Mwamoto ameongeza kwa kusema
ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi
za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
“Mimi nimecheza mpira kwa
mafanikio ndio maana hadi sasa hivi , najua kuwa michezo ni ajira rasmi
hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji chako vizuri”. Mwamoto
Amesema kuwa michezo licha ya
kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa
Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo
seti nzima za Jezi na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na
kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shauku
kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
“Leo nimetoa mipira na jezi hizi
kwa timu za Bomalang’ombe na vijiji vya jirani kwa timu zote za wanaume
na wanawake kwa lengo la kuendeleza vipaji vyenu”alisema Mwamoto
Aidha, amewataka Vijana hao kuwa
na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya
vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha
mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao.
0 maoni:
Chapisha Maoni