Alhamisi, 13 Oktoba 2016

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA AWASILI MKOANI KILIMANJARO – KUKAGUA ENEO LITAKALOJENGWA KIWANDA KIPYA CHA VIATU

Posted by Esta Malibiche on Oct13.2016 in NEWS

min1
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kushoto) akipokea salaamu ya heshima kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro alipowasili Mkoani humo katika ziara ya kikazi ambapo atafanya ukaguzi wa eneo la mradi wa Uwekezaji  wa Kiwanda kipya cha Viatu Gereza Karanga, Moshi ambapo mradi huo ni wa ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa Jamii wa PPF, leo Oktoba 13, 2016.
min2
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo mara baada ya kuwasili Mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi.
min3
Mkuu wa Gereza Kwamugumi, SP. Christopher Mwenda(kushoto) pamoja na  Mkuu wa Gereza Korogwe, ACP. Lenard Mushi wakimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) aliposimama kwa muda kukagua Gereza la Wilaya Korogwe wakati akielekea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro, leo Oktoba 13, 2016 (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

0 maoni:

Chapisha Maoni