Posted by Esta Malibiche on Oct12.2016 in NEWS
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akizungumza na Naibu
Mkurugenzi wa Kitengo cha kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji
wa Binadamu, Carl Fox, baada ya kumtembelea naibu katibu mkuu ofisini
kwake kwa lengo la kujadili ushirikiano wa Tanzania na Marekani katika
kudhibiti biashara hiyo.Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha
kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Carl Fox
akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Balozi Simba Yahya, baada ya kumtembelea Naibu Katibu Mkuu ofisini kwake
kwa lengo la kujadili ushirikiano wa Tanzania na Marekani katika
kudhibiti biashara hiyo. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia
Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka wizarani , Seperatus Fella na
wengine ni wajumbe walioongozana na Naibu Mkurugenzi kutoka ubalozi wa
Marekani. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Kamati ya Kuzuia
Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ,
Seperatus Fella akizungumza na Naibu Mkurugenzi kitengo cha kupambana
na kuzuia usafirishaji binadamu, juu ya hali ya biashara haramu ya
usafirishaji binadamu nchini na namna ambavyo wanashirikiana na taasisi
mbalimbali kuzuia na kutokomeza biashara hiyo. Kikao hicho
kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Kamati ya Kuzuia
Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Seperatus Fella (kulia), akimsikiliza Naibu Mkurugenzi kitengo cha
kupambana na kuzuia usafirishaji binadamu nchini Marekani, Carl Fox,
aliyeambatana na ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani nchini kwa lengo la
kujadili ushirikiano wa Tanzania na Marekani katika kudhibiti biashara
hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
0 maoni:
Chapisha Maoni