Jumanne, 18 Oktoba 2016

WABUNGE VITI MAALUM MKOA WA PWANI WACHANGIA UJENZI WA DARAJA LA USIMBE -MAPARONI WILAYANI KIBITI

Posted by Esta Malibiche on Oct18.2016 in NEWS


mgal1
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Zaynab Matitu  Vullu na  Subira  Khamis Mgalu wakikagua    Ujenzi  wa  Daraja la Usimbe  -Maparoni – Msala wilaya mpya ya Kibiti.
………………………………………………………
  Wabunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Zaynab Matitu  Vullu na  Subira  Khamis Mgalu wamefanya  Ziara   ya Kukagua  Ujenzi  wa  Daraja la Usimbe  -Maparoni – Msala lililopo  Wilaya Mpya ya Kibiti  na  kukabidhi kiasi cha milioni moja 1.000.000/= huku  shilingi milioni  Nne na elfu Hamsini zikiwa zimeingizwa kwenye akaunti na kufanya jumla ya fedha ya mchango walioutoa katika ujenzi wa daraja hilo kufikia  shilingi  Milioni Tano na Elfu Hamsini 5.050.000/=.
Msaada huu unafuatia Ahadi iliyotolewa na Wabunge hao wakati wa Kampeni katika kusaidia Wananchi wa Maeneo ya vijiji hivyo ambao kwa sasa wanatumia Daraja la Muda lililojengwa kwa miti na wananchi wenyewe ili kuwawezesha Kuvuka mto .
Ni muda mrefu sasa hawana daraja ambapo kipindi cha mvua Maji hujaa na kuwapa shida  wananchi hasa Kina Mama Wajawazito na Wanafunzi  hushindwa Kuvuka na baadhi yao wamepoteza Maisha kwa kusombwa na maji kutokana na tatizo la kukosekana kwa  Daraja hilo.
Bajeti ya Ujenzi  wa Daraja  hilo imefika Milioni Kumi   ambapo wabunge hao wamewashukuru  Wadau  wote  waliowaunga   Mkono  katika  kutimiza  Ahadi  hii  ya kusaidia  Wananchi  wa  Vijiji  takriban  saba  hususan  Kina Mama Wajawazito na Wanafunzi ili kuvuka  usalama wanapokwenda  Kupata huduma mbalimbali zikiwemo Afya na Elimu nk.
Wabunge hao waliwaomba wadau mbalimbali walioahidi kuchangia ujenzi wa daraja hilo katika Kata  Mbili  za Maparoni  na Msala na  Wilaya ya Mafia kukamilisha ahadi zao  mungu awajaalie wafanikiwe  kupata chochote ili waweze kuchangia ili tuweze kukamilisha  ujenzi huo ambapo bado unahitaji shilingi milioni 5.000.000 zingine ili kukamilisha bajeti ya ujenzi wa daraja hilo ambayo ni shilingi milioni kumi 10,000.000.
“Tunaamini  mtakapo  pata  fursa  Mtachangia  Mwenyezi  Mungu  Awawezeshe  Amiin” Alisema Mh. Subila Mgalu huku akimaliza kwa  kuwashukuru Viongozi wa Chama, Jumuiya zake , Serikali Ngazi ya Wilaya na Kata kwa mashirikiano makubwa na mapokezi Mazuri . 
Daraja litakapokamilika  litasaidia Vijiji Saba Kipoka , Usimbe ,Maparoni ,Msala ,Twasalie ,Kihasi ,Kiechuru ,Kibanjo Kata Tatu na pia Njia hii inatumiwa Kufika mpaka Mafia. ambapo kwa sasa kumekuwa na athari yingi hasa kwa akina Mama wengi wajawazito wanashindwa kuvuka Maji yanapojaa na kupelekea  kujifungua Njiani.
mgal02
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Subira  Khamis Mgalu akifurahia jambo wakati wa  Ziara   ya Kukagua  Ujenzi  wa  Daraja la Usimbe  -Maparoni – Msala
mgal2
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Subira  Khamis Mgalu wakionyeshwa vipimo vya daraja na  wananchi wakati wa  Ziara   ya Kukagua  Ujenzi  wa  Daraja la Usimbe  -Maparoni – Msala
mgal3
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Zaynab Matitu  Vullu akiwa amekaa na wakina mama wakati wa ziara hiyo wilaya mpya ya Kibiti
mgal4
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Zaynab Matitu  Vullu na  Subira  Khamis Mgalu wakikabidhi fedha taslimu shilingi milioni moja kwa kwa ajili ya   Ujenzi  wa  Daraja la Usimbe  -Maparoni – Msala wilaya mpya ya Kibiti.
mgal8
Hali   ya Vyombo vya Usafiri waliyoikuta wabunge hao wakati walipofanya ziara  Mwaka  Jana  3/10/2015  ambayo iliwagusa  na kuwahamasisha  kutafuta  Michango  ya ujenzi wa daraja hilo Daraja
mgal6
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Subira  Khamis Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.
mgal7
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa  Pwani  Zaynab Matitu  Vullu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.

0 maoni:

Chapisha Maoni