Ijumaa, 14 Oktoba 2016

DKT. SHEIN ASISITIZA WANANCHI KUENDELEA KUPEWA ELIMU YA MPIGA KURA.

Posted by Esta Malibiche on Oct14.2016 in NEWS

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi
mbalimbali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili uwanja wa sabasaba
kutembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi na Vikundi mbalimbali vya maendeleo
ya vijana wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya vijana mkoani humo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akipata
maelezo kuhusu Elimu ya Mpiga Kura
 kutoka
kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bi. Margareth
Chambiri mara baada ya kutembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye viwanja
vya sabasaba wilayani Bariadi uemkoani Simiyu.
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Takwimu
waliokuwa wakitoa Elimu ya Mpiga Kura wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana
Mkoani Simiyu. 
 
Na. Aron Msigwa –NEC, Bariadi-Simiyu.
 
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa elimu ya
mpiga kura inayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika
maeneo mbalimbali nchini ni vema ikawa endelevu kwa kuwa inaongeza uelewa na
kukuza Demokrasia nchini.
 
Dkt. Shein ameyasema hayo
leo mjini Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea banda la maonesho la
Elimu ya Mpiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa kilele cha maadhimisho
ya Wiki ya Vijana na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere
mkoani Simiyu.
 
Amesema hatua ya NEC kuwa
na programu endelevu za kuwapatia wananchi elimu ya mpiga katika maeneo yao ni muhimu
katika kukuza Demokrasia na kuwafanya waelewe wajibu wao katika kudumisha amani
na utulivu nchini kwa kupiga kura kwa uhuru kuwachagua viongozi wanaowataka.
 
“Hongereni sana, mnapotoa
elimu hii mapema mnafanya kazi nzuri, hii inaongeza uelewa miongoni mwa wananchi
na kuwafanya  muwafikie wananchi wengi
zaidi kabla ya uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020” Amesisitiza Dkt. Shein.
 
Kwa upande wake Afisa
Habari Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Margareth Chambiri amemweleza
Dkt. Shein  kuwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi imeshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana mkoani Simiyu ili kutoa Elimu
kwa wananchi hususan vijana wa mkoa huo.
 
“NEC tumeshiriki
maadhimisho haya ili kuwaeleza wananchi namna ambavyo chaguzi mbalimbali zinazofanyika
nchini zinaendeshwa kwa uhuru na uwazi kabisa, katika kufanikisha jambo hili
Idara mbalimbali zimeshiriki ikiwemo Idara ya Elimu ya Mpiga Kura, Idara ya TEHAMA,
Idara ya Daftari la Wapiga Kura, Idara ya Uchaguzi na Idara ya Sheria” Ameeleza
Bi. Margareth.
 
Amesema tangu kuanza
kwa maonesho hayo Oktoba 8, mwaka huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imefanikiwa kutoa Elimu ya Mpiga kura kwa wananchi waliokuwa wakilitembelea
banda la maonesho la NEC, kutoa elimu hiyo kupitia majukwaa ya wazi ya burudani
pamoja na kutoa elimu ya mpiga kura kwa wanafunzi wapatao 2100 wa shule za
Sekondari mkoani humo.

0 maoni:

Chapisha Maoni