Na Woinde Shizza,Arusha
Mkurugenzi wa
halmashauri ya jiji la Arusha, Athumani Kahamia ametoa ufafanuzi kuhusu
tuhuma ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha sh, 500 milioni
zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri
ya Kaliua na kusema kwamba fedha hadi anahamishwa fedha hizo hazikuwahi
kuletwa katika halmashauri hiyo kutoka serikali kuu.
Hivi karibuni kumekuwa
na tuhuma mbalimbali zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini
ambapo Kahamia anatuhumiwa kutumia kiasi hicho cha fedha zilizotengwa
kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Kaliua
wakati akiwa mkurugenzi wa Kaliua kabla ya kuhamishiwa jijini Arusha.
Akihojiwa na mwandishi
Wa Habari hizi Kahamia alisema kwamba aliripoti mnamo febuari 2015
katika halmashauri hiyo na kukuta ujenzi wa jengo la utawala ukiendelea
ambapo katika bajeti ya halmashauri ya Kaliua mwaka wa fedha 2015/16
waliomba fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo katika awamu ya
kwanza lakini serikali haikuleta pesa hizo.
Alisema ya kwamba
lakini pamoja na kutenga bajeti ya fedha hizo halmashauri hiyo
haikupokea kiasi hicho kutoka serikali kuu na kusisitiza kwamba hadi
anaondoka Kaliua fedha hizo hazikuwahi kuzipokea.
“Hadi tarehe 30 juni
mwaka huu hizo fedha tulikuwa bado hatujazipokea mpaka leo tunavyoongea
hizo fedha hazijapokelewa taarifa kwamba nimezitafuna zinalenga
kunichafua “alisema Kahamia
Hatahivyo, alifafanua
tuhuma kwamba tayari ameandikiwa barua ya kurudishwa Kaliua ili kujibu
tuhuma zinazomkabili na kusema si kweli kwani hadi sasa hajapokea barua
yoyote wala wito kutoka mamlaka yoyote kumtaka arudi kujibu madai hayo.
Hatahivyo, alifafanua
tuhuma za kumwingilia mkandarasi kutoka kampuni ya Saram Company Limited
iliyopewa zabuni ya kujenga jengo hilo la utawala na kusema yeye kama
mwajiri alivunja mkataba na kampuni hiyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa
mkandarasi huyo alionekana kusuasua katika majukumu yake.
Alisema kwamba baada ya
mkandarasi huyo kuonyesha udhaifu katika mkataba wake walimpa onyo na
kisha nitosi kabla ya kuvunja mkataba wake ambapo alikimbilia mahakamani
lakini walimshinda kesi hiyo.
“Huyu mkandarasi
alipaswa kumaliza kazi mwezi Mei mwaka 2015 lakini hadi Septemba mwaka
huo alikuwa bado hajamaliza kazi yake ndipo tukavunja mkataba wake
Akakimbilia mahakamani tukamshinda akakata rufaa tukamshinda tena mchezo
ukaishia hapo hapo “alisema Kahamia
Alisema kwamba wakati
wa kuvunja mkataba na mkandarasi huyo zoezi hilo lilisimamiwa na timu ya
wanasheria wa halmashauri ya Kaliua pamoja na mkaguzi wa ndani chini ya
usimamizi wa mkuu wa mkoa wa Tabora wakati huo, Ludovick Mwananzila.
Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Kaliua, Haruna Kasele alipoulizwa kuhusu tuhuma
hizo kwa njia simu alisema kwamba ni kweli halmashauri hiyo katika
bajeti ya mwaka 2015/16 waliomba kiasi cha sh,500 milioni kwa ajili ya
ujenzi wa jengo hilo lakini hadi mwaka wa fedha wa serikali unakwisha
hawakuwahi kupokea fedha hizo.
Hatahivyo,alithibitisha
taarifa za halmashauri hiyo kuvunja mkataba na mkandarasi huyo chini ya
baraza la madiwani na kusema sababu iliyopelekea ni baada ya mkandarasi
huyo kusuasua na kushindwa kumaliza kazi aliyopewa kwa wakati mwafaka.
Kuhusu madai ya Kahamia
kuandikiwa barua ya kuitwa ili kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo mwenyekiti
huyo alisema kwamba hakuna jambo kama hilo na wala hawajaandika barua ya
kumwita kumhoji mkurugenzi huyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni