Posted by Esta Malibiche on Oct 29.2016 in NEWS
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiendelea na kazi ya kuchambua
maoni yaliyotumwa na wadau wa habari ili kuboresha Muswada wa Sheria ya
Huduma za Habari leo mjini Dodoma.
(Picha na MELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii inaendelea na kazi yao ya kutunga Sheria ya
Huduma za Habari kwa kutumia maoni yaliyowasilishwa na wadau mbalimbali
na kuwasilisha Serikalini kabla ya kupelekwa Bungeni ili muswada
ukajadiliwe na Wabunge na hatimaye kupatikana Sheria ya Habari ambayo
inalenga kuleta heshima kwa Watanzania.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.
Peter Serukamba amebainisha hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari kabla ya Kamati hiyo kuendelea na kazi
yake ya kuchambua maoni yaliyotumwa na wadau wa habari ili kuboresha
Muswada huo kabla ya kuwasilishwa Bungeni kusomwa kwa mara ya pili.
Serikali imekuwa ikiwasikiliza
wadau wa habari kwa muda mrefu licha ya kuwa na tabia ya kutokuwasilisha
maoni yao kila mara wanapoomba kupewa muda wa kutoa maoni yao juu ya
kuboresha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari nchini.
“Ni vizuri ifahamike, huu ndio
umekuwa mchezo wa Muswada huu tangu mwaka 1993, kila mara Muswada
ulipokuja Bungeni, wadau walisema hawapo tayari wanasema utoke” alisema
Mhe. Serukamba.
Aidha, Mhe. Serukamba amesisitiza
kuwa huo umekuwa ni mtindo wa wadau hao kwa miaka zaidi ya 22 sasa
ambapo Serikali imekuwa imekuwa ikiwasililiza kila waliposema hawapo
tayari, muswada huo ulitolewa Bungeni.
Kufuatia tabia ya wadau
kutokuwasilisha maoni yao kwa kisingizio cha kutopewa muda Mhe.
Serukamba amesisitiza kuwa kamati itaendelea kujadilia maoni
yaliyowasilishwa kwako na kuahidi kutunga Sheria itayozingatia na kujali
maslahi ya wadau wote wa habari ili kuufanya Muswada huo kuwa wenye
tija kwa wananchi na taifa kwa kuleta mabadiliko katika tasnia ya
habari nchini.
Ili kusimamia nia na maslahi ya
wadau na taifa, Serikali imeuleta tena Muswada huo Bungeni ambapo Kamati
ya Huduma za jamii inaendelea kuujadili na kuchambua maoni
yaliyowasilishwa na wananchi pamoja na wadau wa habari kwa njia
mbalimbali ikiwemo kwa maandishi kupitia barua pepe ya Bunge cna@bunge.go.tz
Mwenyekiti wa Kamati hiyo
amewataja wadau waliothibitisha kupokea barua ya mwaliko wa kuleta maoni
yao kwa Kamatikuwa ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS),
MCT, LHRC, UTPC pamoja na Pili Mtambalike.
0 maoni:
Chapisha Maoni