Posted by EstaMalibiche on Oct 3.2016 in NEWS
Katibu wa chama cha walimu mkoani
Pwani, (CWT),Nehemiah Joseph ,akizungumza kuhusiana na wizi uliotokea
katika jengo la chama hicho ,ambapo computer za mezani na mpakato 11
zimeibiwa na zaidi ya mil.5 .(picha na Mwamvua Mwinyi).
………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
OFISI sita zilizopo jengo la
chama cha walimu mkoani Pwani(CWT)zimevunjwa na kuibiwa Kompyuta za
mezani na mpakato 11 zinazodaiwa kufikia sh.mil 15 na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Mbali ya kuibiwa vitendea kazi
hivyo,watu hao pia wamechukua kiasi cha fedha taslimu sh. mil 5,036,515
zilizokuwepo katika baadhi ya ofisi hizo.
Kufuatia tukio hilo, jeshi la
polisi mkoani Pwani,linawashikilia walinzi wawili wa jengo hilo kutoka
kampuni ya Noble security Tanzania ltd ya Kibaha,Hamad Kisoki(32)mkazi
wa Mailmoja na Said Mohammed (39) mkazi wa Mwanalugali.
Akizungumzia kuhusiana na tukio
hilo,katibu wa CWT mkoani humo,mwl Nehemiah Joseph,alisema tukio
limetokea usiku wa octoba mosi kuamkia octoba 2 mwaka huu.
Alisema siku ya tukio walinzi
waliotakiwa kuingia kazini walikuwa ni wawili lakini badala yake
aliingia mmoja ambae ni Said Mohammed .
“Ambapo alipokuwa kwenye lindo
anadaiwa kupatiwa chips na kinywaji aina ya juise vinavyosemekana kuwa
na madawa ya kulevya kutoka kwa mwanamke asiyefahamika”.alisema.
Mwl.Joseph alielezea kuwa ,baada
ya kupatiwa chakula hicho mlinzi alipoteza fahamu na hivyo kutoa mwanya
kwa watu hao walivunja milango ya ofisi hizo na kuingia bila bughudha .
Alisema inadaiwa mwanamke
aliyempatia chakula aliihitaji kuwapa chakula walinzi hao wote wawili
kabla Mohammed hajaachiwa lindi lakini mwenzie Hamad alikataa na kusema
anaenda kula nyumbani.
Mwl.Joseph alisema mwanamke huyo
kwa hali ya kawaida atakuwa ni mmoja kati ya watu hao kwani haiwezekani
ampatie mtu chakula kisha apate madhara na kutokea wizi huo.
Alizitaja ofisi zilizopo kwenye jengo la CWT mkoa ambazo zimeibiwa ni pamoja na CWT mkoa computer 1 na fedha sh.mil 1.532,CWT wilaya computer 2 na mil moja,beem financial services (BFS) computer moja na mpakato(laptop) moja.
Ofisi nyingine ni Chodawu
computer 2 na mpakato moja,Tuico computer 1 na mpakato moja pamoja na
fedha ,mil.1.170 na TCCIA iliyoibiwa computer moja na fedha
mil.1,334,515.
Katibu huyo wa CWT mkoani
hapo,alieleza kwasasa wameshafikisha taarifa hizo jeshi la polisi wilaya
na mkoa kwa hatua zaidi na ofisi ya chama hicho imeshakaa na taasisi
zote zilizopanga jengo hilo kufanya tathmini.
Mwl.Joseph alisema kampuni ya
Noble Security waliingia nayo mkataba hivyo baada ya kufanyika tathmini
wataipatia ili kuangalia namna ya kulipia gharama zilizotokea.
“Inasikitisha sana kutokea kwa
wizi huu lakini kwa hili iwe fundisho kwa walinzi wengine,waache kula
kula ama kununua vyakula kwa watu wasiowajua,kwani kwa kufanya hivyo
kunasababisha kuwapa upenyo wahalifu na kuletea hasara kwa wenye
mali”alisema mwl Joseph.
Kwa upande wake,kamanda wa polisi
mkoani Pwani,Boniventure Mushongi ,alikiri kutokea kwa tukio hilo usiku
wa kuamkia octoba 2 (jumapili).
Mushongi alisema majira ya saa 5
asubuhi walipata taarifa za kuvunjwa kwa jengo hilo kutoka kwa Elizabeth
Thomas ambae ni katibu wa chama hicho wilaya ya Kibaha huko mkoani A
,kata ya Tumbi.
Hata hivyo ,Kamanda huyo alisema
,baada ya kufanya wizi huo watu hao walitokomea kusikojulikana na jeshi
hilo bado linawatafuta,huku akiomba ushirikiano kwa jamii kuwafichua
watu wanaowadhania kuhusika na wizi huo.
Alisema kwasasa wanawashikili
walinzi wawili kati ya walinzi wanaolinda jengo hilo kwa ajili ya
uchunguzi juu ya wizi uliotokea.
Mushongi aliwaasa walinzi na
wafanyakazi katika maofisi na taasisi mbalimbali mkoani humo,kuacha
tabia ya kununua vyakula ama kupewa vyakula na mtu au watu wasiowajua
ili kuepukana na madhara yoyote ikiwemo kuwekewa madawa ya kulevya .
0 maoni:
Chapisha Maoni