Ofisa
Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar
Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga
tabia ya kutumia Kingatiba ya magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo,
Usubi Matende na Mabusha wakati wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari,
Dar es Salaam leo. Kampeni ya kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi
takribani mil. 4 wa Jiji la Dar es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu.
Meneja Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Upendo Mwingira akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo.
Mtangazaji
wa BBC, Halima Kassim akitafakari jambo kuhusu semina hiyo ya
wanahabari kupata uelewa kuhusu magonjwa hayo na jinsi ya kuwaelimisha
wananchi kutumia Kingatiba kwa kumeza dawa mara noja kila mwaka ili
kuboresha afya.
Mtaalamu Kaitaba akionesha baadhi ya dawa za Kingatiba ya magonjwa hayo.
Ofisa
Habari wa Mradi huo, Said Makora akiwataka wanahabari kuwaelimiasha
wananchi juu ya magonjwa hayo na jinsi ya kupata Kingatiba kwa kuandika
makala, habari, majarida na kutumia mitandao ya kijamii kwa nia ya
kuyatokomeza magonjwa hayo kufikia mwaka 2020.
Kaitaba akionesha vifaa vinavyotumika kuwapima watu ili wapewe dawa kulingana na kimo chake.
Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Jasmin akichangia mada wakati wa semina hiyo.
Wana habari wakipatiwa dawa za Kingatiba za magonjwa hayo.
Mtangazaji wa E FM Radio akipimwa urefu ndipo apatiwe dawa .
0 maoni:
Chapisha Maoni