Posted by Esta Malibiche on Oct 22.2016 in NEWS
Mgeni Rasmi Mhe. Mahmoud Thabit
Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (mwenye kaunda
suti ya kijivu) akiwa katika Jukwaa Kuu na viongozi waandamizi kutoka
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania pamoja na viongozi kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani
(UNFPA). Wengine pamoja nae ni Bw. Barnabas Yisa, Ofisa Mkaazi Mfawidhi
UNFPA Tanzania (kushoto) na Mhe. Issa Juma Ally, Mkuu wa Wilaya ya
Kaskazini B (kulia).
Mhe. Salama Abuu Talib, Waziri wa
Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Wizara
ya Fedha na Mipango, Zanzibar akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe
hizo.
Wananchi wa kijiji cha Kilombero,
Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia kwa makini
yaliyokua yakijiri wakati hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo.
Bw. Barnabas Yisa, Ofisa Mkaazi
Mfawidhi UNFPA (mwenye shati jeupe) akitoa neno kwa wananchi
walioshiriki shughuli ya uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu
Duniani. Kushoto ni Bibi. Christina Mwanukuzi Kwayu, Mwakilishi
Msaidizi, UNFPA akitafsiri kwa lugha ya kiswahili hotuba ya Ofisa Mkaazi
Mfawidhi.
Mhe. Issa Juma Ally, Mkuu wa
Wilaya ya Kaskazini B, akitoa neno kwa wananchi waliohudhuria uzinduzi
wa Taarifa hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kuongea na
wananchi na kuizindua rasmi.
Mgeni Rasmi Mhe. Thabit Kombo,
Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akieleza juu ya fursa
ndogo waliyonayo wasichana ya kumaliza skuli kuliko wavulana na wako
katika hatari zaidi ya kukabiliwa na ndoa za utotoni, ajira za watoto,
ukeketaji na matendo mengine ya udhalilishaji.
Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa
Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akikata utepe kuashiria uzinduzi
rasmi wa Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani.
Mgeni Rasmi Mhe. Thabit Kombo,
Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwaonyesha wananchi
kitabu cha Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani mara baada ya
kuizindua.
0 maoni:
Chapisha Maoni