Posted by Esta Malibiche on Oct14.2016 in NEWS
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo, akiongea na watumishi wa Halmashauri wa Babati. |
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo
amekemea tabia iliyokuwa ikifanywa awali na baadhi wa watumishi wasio
waadilifu kwa kuchukua rushwa kwa wakandarasi wa miradi ya ujenzi kwa
kuwalazimisha kutoa fedha ili kupewa kazi na kuidhinishiwa malipo yao.
Jafo alisema kwamba kumekuwa na
tabia ya “Utatu usio mtakatifu ” katika halmashauri ambo una athiri sana
utekelezaji wa miradi ya ujenzi.
Utatu huo unawahusisha Afisa
Manunuzi, Mhandisi wa ujenzi, na mweka Hazina (DT), ambapo Jafo alisema
kwamba halmashauri ikiwa na kazi ya ujenzi Afisa Manunuzi anaweza
mazingira kupata fedha ili mkandarasi apewe kazi.
Mkandarasi akishapata kazi
anakutana na kizingiti kingine kutoka kwa Mhandisi (Engineer) ambaye
anagoma kupitisha certificate yeyote ya kazi iliyofanyika mpaka apewe
chake mapema.
Kizingiti cha tatu kinajitokeza
pale Mweka Hazina (DT) kugoma kuandaa malipo na kutoa cheki ya
mkandarasi hadi apewe chake. Haki hii inamfanya Mkandarasi wa ujenzi
anajikuta ametoa fedha nyingi ili apate kazi na kupokea malipo.
Kutokana na Utatu huo, umesababisha baadhi ya miradi kujengwa chini ya kiwango hivyo kuharibika baada ya kipindi kifupi.
Jafo alikemea tabia hiyo alipokuwa
akikagua miradi ya maendele na kuongea na watumishi wa halmashauri za
wilaya ya Babati, Mbulu, Nzega, Igunga na Iramba.
Aliwataka wafanyakazi wa halmashauri kufanya kazi kwa kujiamini na kuzingatia kanuni za utumishi wa umma.
Aliwaagiza wakurugenzi kukuza
vipaji vya watendaji wao kwani wengi wao japo ni wasomi wazuri lakini
wamekuwa hawatumiki vyema na baadhi yao kutopewa kipaumbele katika idara
zao.
Naibu Waziri wan chi, Ofisi ya
Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo, akiongea na
kina mama wajawazito wanaosubiria kujifungua katika jengo maalum kwa
kinamama wanaotoka mbali ili kuepuka vifo vya kinamama wakati wa
kujifungua katika hospitali ya Iramba, Singida.
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo,akikagua
hospitali ya wilaya ya Iramba mkoani Singida.
0 maoni:
Chapisha Maoni