Ikiwa ni wiki moja tangu staa wa Barcelona, Neymar kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumia Barcelona hadi mwaka 2021, baba yake mzazi, Neymar Santos Sr amefunguka ni jambo gani hasa ambalo linachangia kumfanya mtoto wake kutaka kuendelea kuitumikia Barcelona.
Santos ameeleza kuwa siri ya mtoto wake kuongeza mkataba kuichezea Barcelona ni Messi, kwani mchezaji huyo amekuwa mtu ambaye anamhamasisha mtoto wake kucheza vizuri na ndie mchezaji anayempenda zaidi dunianii hivyo kuwa timu moja na Messi kwake ni jambo lenye thamani kubwa.
“Wote tunamjua Messi ni nani na ana maana gani, Messi ni mtu ambaye mwanangu anamwangalia na kwake ni jambo la heshima kucheza karibu na yeye,” alisema Neymar Sr. na kuongeza.
“Ana furaha kucheza nae pamoja na anacheza hapa [Barcelona] kwa ajili ya Messi, kama ukiwataja Messi na Ronaldo huwezi kuacha kumtaja Neymar, kama ilivyo kwa Pele na Maradona, wote wamekuwa wakiwahamasisha wachezaji wengi”