Posted by Esta Malibiche on
News
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi saba Barani
Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi hivyo amewakaribisha
wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.
Tanzania
ni nchi ya pili kwa kasi ya ukuaji wa uchumi Barani Afrika ambapo
uchumi wake unakuwa kwa asilimia 7 ikiongozwa na Ivory Coast inayokua
kwa asilimia 8.5, Senegal ya tatu (asilimia 6.6), D’jibout ya nne
(asilimia 6.5), Rwanda ya tano (asilimia 6.3), Kenya ya sita (asilimia
6.0) na Msumbiji ya saba (asilimia 6.0).
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamis, Oktoba 13, 2016) wakati
akifungua kongamano la Jumuiya ya Dawoodi Bohora lililohusu fursa za
uwekezaji.
Amewakaribisha
wanajumuia hiyo kuja kuwekeza nchini. Kongamano hilo lilifanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere.
“Tanzania
ina sera nzuri za kiuchumi ambazo zimesababisha uchumi wake kuendelea
kuwa imara kwa zaidi ya miongo miwili sasa. Naikaribisha jumuiya ya
Bohora kuja kuwekeza na kufanya biashara Tanzania,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema makampuni yatakayowekeza nchini yatafaidika na uwepo wa
malighafi za kutosha, sera nzuri uwekezaji pamoja na uhakika wa usalama
wa mali zitakazowekezwa nchini kwa sababu ya hali ya amani na utulivu
iliyoko nchini.
Alisema
licha ya Tanzania kuwa maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji pia ina
soko la uhakika kwa sababu ya kuwa mwanachama wa jumuiya mbili ambazo ni
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) zenye watu takriban milioni 600.
“Tanzania
ni kitovu cha biashara kwani inapakana na nchi nane ambazo kati yake
nchi sita zinatumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo yake.
Mizigo hiyo husafirishwa kwa njia ya reli na barabara,” alisema.
Nchi
zinazopakana na Tanzania ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi,
Zambia, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Zinazotumia
bandari ya Dar es Salaam ni Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Malawi na
Zambia.
Kwa
upande wake Mratibu wa Kongamano hilo la kidini (Ashara Mubarak)
lililowakutanisha Mabohora kutoka duniani kote Bw. Murtaza Adamjee
ameahidi kushirikiana na Serikali katika kutangaza fursa za uwekezaji
zilizoko nchini.
Bw.
Adamjee alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba Mabora dunia nzima wanakuja
Tanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali hususan ya viwanda.
“Tutafikisha ujumbe kwa Mabohora dunia kote kwamba Tanzania ni sehemu
salama ya kuja kuwekeza,”
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akitoa hutuba katika kufunga kongamano hilo jioni ya jana Oktoba 13.2016, Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ukiendelea
0 maoni:
Chapisha Maoni