TABIA ya vijana kutojishughulisha katika miradi mbalimbali yenye tija kumeeelezwa kuwa moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi, mkoani Simiyu.
Alisema kumeanza kujitokeza hali ambapo vijana nchini kutokupenda kujishughulisha katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na hivyo kushindwa kuondokana na umaskini na pia kuchangia katika pato la taifa.
Alisema kuwa vijana wanaongoza kwa idadi kubwa lakini wanashindwa kujishughulisha kuhakikisha wanapata maendeleo ambayo yanaweza kulisaidia taifa.
img_0053Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida (kushoto) akisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama (kulia) alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi, mkoani Simiyu kufungua kongamano la vijana.

img_0055Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake Mh. Anthony Mavunde wakisalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na ESRF mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi, mkoani Simiyu.
Alisema zaidi kwamba wanalengo la kuhakikisha mkoa unaingia katika tano bora ya uchangiaji wa pato la taifa.
Amehimiza viongozi kuwasaidia vijana kuwaongoza, kuwaelekeza na amewataka vijana kuwa na uthubutu na kuungana kwa pamoja.
Pamoja na harakati za kiuchumi vijana wametakiwa kuwa na mwendo wenye maadili mema ili kuendelea kuwa na afya bora na kukwepa magonjwa yanatokanayo na ukosefu wa maadili.
 Amesistiza kuwa kauli mbiu waliyoanzisha ya “Bidhaa moja,wilaya moja” itumike ipasavyo ili kufanikisha maendeleo yao na ya wilaya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi, mkoani Simiyu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida  alisema ushiriki wa vijana katika viwanda vidogovidogo kunaweza kukuza uchumi kutokana na viwanda hivyo kutoa ajira na pia kutengeneza mnyororo wa thamani katika mazao ya wakulima ambako vijana ndiko wanakotarajiwa kuonesha ushujaa wao.
Hata hivyo alisema ukuaji wa uchumi kwa sasa bado ni changamoto kwa wananchi wanaoishi vijijini kutokana na baadhi ya huduma kutowafikia kwani asilimia 7 inayopanda kiuchumi huwa haitafsiriki  kufikia makundi yote ya kijamii .
“Tumekuwa tukiendesha tafiti nyingi lakini tunaona kipato chetu kinaendelea kushuka hasa katika wananchi wanaoishi vijijini hivyo kuwepo kwa viwanda kutaweza kuwainua kiuchumi wananchi kutokana na bidhaa zao ghafi kuuzwa katika viwanda”Alisema  Dk. Kida.
Nao wafadhili wa Kongamano hilo UNDP wamesema wametenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana katika programu zao za maendeleo.
img_0183Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mhagama.
img_0209Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza machache awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama kufungua kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi, mkoani Simiyu.
img_0248Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu kwa vijana kutoka visiwani Zanzibari kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0098Meza kuu mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani ( wa pili kulia), Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida (kushoto), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa tatu kushoto).
img_0200Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mpiango, Mudith Cheyo (kulia) na Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0446Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akiwasilisha mada ya mageuzi ya kiuchumi yanayohitajika kuboresha maisha ya vijana pamoja na hali ya uchumi nchini kwa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini walioshiriki kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0415
img_0470Bw. Abdallah Hassan (kushoto) na John Kajiba wa ESRF wakifuatilia jambo kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0653Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo UNDP, Amon Manyama akizungumzia mchango wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN/UNDP) katika Maendeleo Endelevu ya Vijana wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0134Sehemu ya umati wa vijana na wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0481Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy akiwasilisha mada ya fursa za vijana katika uchumi wa viwanda pamoja na Mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21 kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0773Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Dotto akiwasilisha mada iliyozungumzia mchango wa elimu ya ufundi stadi katika kufikia Tanzania ya viwanda katika kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0728Afisa Mwandamizi wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Abdallah Hassan akizungumzia fursa mpya ya kilimo biashara kwenye kongamano la vijana Simiyu,  lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0905Pichani juu na chini washiriki wakiuliza maswali kwa wakufunzi na viongozi wa serikali katika kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0929
img_0154Pichani juu na chini ni umati wa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Vyuo Vikuu waliohudhuria kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0162
img_0164
img_0855
img_0595Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake, Mh. Anthony Mavunde katika picha ya pamoja na mdhamini mkuu wa kongamano hilo UNDP, waratibu ESRF pamoja na wawasilishaji mada kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi, mkoani Simiyu.
img_0578Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka katika picha ya pamoja na wawasilishaji mada, ESRF pamoja na UNDP kwenye mabango ya viwanda vilivyoanzishwa na vijana cha Meatu Milk na kiwanda cha kwanza Tanzania cha kutengeneza Chaki cha mkoani Simiyu.
img_0124
img_0143Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde wakimtunza mwanakikundi wa ngoma za asili cha Wanaisanga kutoka Maswa mwenye uzoefu wa kucheza na Chatu wakati wa burudani kwenye kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0014Mwanakikundi wa ngoma za asili cha Wabonyangi kutoka Maswa mwenye uzoefu wa kucheza na Chatu akionyesha umahiri wake wa kucheza na chatu kwenye kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
img_0037Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy, Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama, Mtafiti Mshiriki ESRF, Dr. Oswald Mashindano, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dr. Tausi Kida, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ESRF, Margareth Nzuki wakifurahi burudani ya ngoma za asili ya kucheza na Chatu wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Alliance mjini Bariadi.
img_0035Wageni waalikwa wakiendelea kufurahi burudani ya ngoma za asili kwenye kongamano la vijana Simiyu.
img_0902Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kongamano la vijana Simiyu waliwakilisha.