Posted by Esta Malibiche on Oct 28.2016 in NEWS
Kamishna Jenerali wa Magereza,
CGP- John Casmir Minja akisalimiana na baadhi ya Maafisa Watendaji
katika mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula,
Mkoa wa Pwani leo Oktoba 28, 2016 alipotembelea mradi huo ili kujionea
shughuli za uzalishaji wa kokoto.
Meneja Msaidizi wa Mradi wa
Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula, Kepteni Gaspa
Rugayana akitoa maelezo mafupi kuhusiana na mradi huo kwa Kamishna
Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia).
Ujumbe wa Maafisa Watendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(Prisons Corporation Sole)
ambao umefuatana na Kamishna Jenerali wa Magereza katika ziara ya
mafunzo kwenye mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe
Msungula, Mkoa wa Pwani. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza
linatarajia kuanzisha mradi wa Uzalishaji kokoto katika eneo la Gereza
Msalato, Mkoani Dodoma.
Maafisa Watendaji wa SUMA – JKT
katika mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula
wakimtembeza katika maeneo mbalimbali Kamishna Jenerali wa Magereza,
CGP- John Casmir Minja(wa tatu kulia) alipofanya ziara ya mafunzo katika
mradi huo(kulia) ni Meneja Fedha na Utawala katika Mradi huo, Bi. Glory
Kimaro.
Meneja Uzalishaji wa mradi wa
kokoto, Kepteni Paul Mbeya akimuonesha mtambo wa uzalishaji kokoto
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia).
Mtambo wa Uzalishaji katika mradi
wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula kama
unavyoonekana katika picha. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza
linatarajia kuanzisha mradi wa Uzalishaji kokoto katika eneo la Gereza
Msalato, Mkoani Dodoma.
Meneja Mkuu wa Mradi wa Uzalishaji
kokoto wa SUMA – JKT, Bw. Semih Yaran akimuonesha Kamishna Jenerali wa
Magereza, CGP- John Casmir Minja(wa pili kulia) maeneo mbalimbali ya
mradi huo.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
0 maoni:
Chapisha Maoni