Posted by Esta Malibiche on Oct 23.2016 in MICHEZO
Timu
ya Chelsea imeibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 kwa kuwafunga
Man United ya Kocha Jose Mourinho ambaye alitimuliwa mwaka jana na
Chelsea hivyo leo ilikuwa mara ya kwanza kukanyanga uwanja wa Stamford
Bridge mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza na hiki ndicho kipigo kikubwa
msimu huu kukipata mashetani hao.
Pedro alikuwa wa kwanza kuipatia goli
timu yake dakika ya mapema ya pili kwa pasi ya Marcos Alonso baada ya
kufungwa Man United walikuwa juu huku wakiwa wakitumia style ya
kushambulia na kujilinda na dakika ya 21 walifungwa goli la pili
likifungwa na beki kisiki Gary Cahill kwa kichwa hadi mapumziko wenyeji
walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa Chelsea
kuendelea kulishambulia lango la Man United,licha ya mashetani hao
kumiliki mpira kwa asilimia kubwa walijikuta wakifungwa goli la tatu
kupitia kwa winga hatari Eden Hazard dakika ya 62 kuingia kwa goli hilo
liliwachanganya vijana wa Mourinho na katika dk ya 70 kiungo
aliyesajiliwa kutoka kwa Leicester City N’golo Kante alifunga goli la
nne huku likiwa la kwanza kwake msimu huu.
Chelsea wakitumia mfumo wa mabeki watano
nyuma uliwapa wakati mgumu Man United na kujikuta wakizidiwa kila idara
ya mchezo na kucheza mpira wa ovyo na kujichanganya na kushindwa kujua
namba fulani anacheza nani na kwa matokeo hayo Chelsea wanapanda hadi na
nafasi ya nne wakiwa na pointi 19 wakati Man United wameshuka hadi
nafasi ya mtaa wa saba yaani ya saba kwenye msimamo.
0 maoni:
Chapisha Maoni