Katika
kuhakikisha magonjwa yatokanayo na Pneumococcal yanatoweka duniani,
waalamu wa afya kutoka nchi mbalimbali Afrika na watengenezaji wa chanjo
inayotumika kukinga watoto na magonjwa mbalimbali kama Nimonia
wamekutana katika mkutano wa siku tatu wa Kanda ya Afrika uliyo na
malengo ya kujadili magonjwa yanayotokana na Pneumococcal.
Magonjwa
ambayo yanatona na Pneumococcal ni pamoja na Nimonia (homa ya mapafu),
homa ya uti wa mgongo na maambukizi ya damu ambapo wataalamu hao na
watengenezaji wa damu kwa pamoja watajadili jinsi gani wanaweza
kutokomeza magonjwa hayo katika nchi zao.
Akizungumza
na MO BLOG, Meneja wa Taifa wa Mpango wa Chango kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dafrossa Lyimo amesema
mkutano huo utaweza kusaidia kuona ni jinsi gani wataweza kutokomeza
kabisa magonjwa yanayotokana na Pneumococcal na zaidi ugonjwa wa Nimonia
licha ya takwimu kuonyesha kuwa kwasasa Tanzania inafanya vizuri.
Meneja
wa Taifa wa Mpango wa Chango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dafrossa Lyimo akizungumza kuhusu mkutano huo
na kutoa takwimu za Tanzania.
Amesema
pamoja na mafanikio ambayo wameyapata lakini bado wanataka kuhakikisha
wanaondoa kabisa uwezekano wa ugonjwa huo kuwapata watoto ambao wamekuwa
wakipatiwa chanjo tangu wawapo watoto wachanga.
“Tumekuwa
tukipokea chanjo kutoka shirika la GAVI ambazo tumekuwa tukigawa nchi
nzima ili kila mtoto aweze kupata, sisi tunachukua chanjo Milioni 1.9
kwa mwaka na takwimu zetu zinaonyesha watoto 97% wamekuwa wakipata
chanjo na kwasasa tunajiuliza jinsi gani tutakamilisha ifike 100,
“Changamoto
ambayo inajitokeza ni wazazi wengine kutokupeleka watoto wakapate
chanjo, wengine wanawapa mara moja au mbili na hii chanjo mtoto
anatakiwa kuipata mara tatu, wiki ya sita tangu azaliwe, wiki ya kumi na
wiki ya 14,” alisema Dafrossa.
Mkurugenzi
Mwandamizi wa Shirika la Pfizer, Heather Sings akielezea sababu ya
kuandaa mkutano huo na malengo ambayo watayaweka baada ya mkutano.
Aidha
aliwataka wazazi kuwa wakiwapeleka watoto katika chanjo kwani madhara
ambayo yanaweza kujitokeza ni makubwa na ambayo yanaweza kusababisha
wakasimama kufanya shughuli za kiuchumi kwa ajili ya maisha yao na
kuanza kuhangaika kupata matibabu ambayo kama wangezingatia mapema
wangeweza kujiepusha na hilo.
Tanzania
ilianza kutoa chanjo ya PVC13 ya kujikinga na Nemonia kwa watoto kutoka
Shirika la GAVI tangu Januari, 2013 na GAVI inataraji kusitisha kutoa
msaada huo mwaka 2025 hivyo nchi za 18 za Afrika ambazo zinapokea msaada
huo zimetakiwa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kujinunulia dawa pindi
misaada ya chanjo hiyo itakapomalizika.
Mkurugenzi
wa Sayansi wa Shirika la AMP, Dk. Bradford Gessner akielezea moja ya
mada ambayo wanazijadili katika mkutano huo wa siku tatu.
Baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.
0 maoni:
Chapisha Maoni