Jumapili, 23 Oktoba 2016

SIMBA YATAFUNA TOTO LA YANGA,MZAMIRU NA MAVUGO WAPELEKA KILIO MWANZA.

unnamed

Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

Simba imeendeleza rekodi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kupata ushindi wa 11 bila kufunga pamoja na kuvunja mwiko wa Toto baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Mzamiru Yassin aliye kwenye kiwango bora kwa sasa alianza kuifungia timu yake bao la kwanza mnamo dakika ya 43 baada ya kazi nzuri kutoka kwa mshambuliaji matata,Fredrick Blagnon kuwachachafya mabeki wa Totoi na kutoa pasi kwa mfungaji hadi mapumziko Mnyama alikuwa mbele kwa bao moja.

Simba walipata pigo baada ya Blagnon kuumia kutokana kugongana na mchezaji wa Toto na kusababisha kutolewa nje na nafasi yake kuchuliwa na Laudit Mavugo,mnamo dakika ya 52 Mavugo aliiandikia goli la pili huku likiwa la nne kwenye Ligi baada ya kuingia kwa goli hilo liliwachanganya wageni na kuanza kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango lao huku wao wakikosa umakini wa kutafuta hata bao la kufutia machozi.

Kwa ujumla timu zote ziliendelea kushambuliana huku Simba wakiliandama lango la wageni kama nyuki Mzamiru tena alirudi kwenye nyavu kwa kufunga goli safi la tatu na likiwa la nne kwake na kuendelea na nyota ya kufumania nyavu akifanya hivyo dhidi ya Mbao Fc.

Hadi mwamuzi anamaliza mpira Simba wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kwa matokeo hayo Mnyama anaendelea kung’ang’ania kileleni mwa Ligi kwa kufikisha pointi 29 kwa kucheza michezo 11 huku akiwa bado hajapoteza hata mchezo mmoja wakati Toto wanabaki mkiani wakiwa na pointi 8.

0 maoni:

Chapisha Maoni