Posted by Esta Malibiche on Oct8.2016 in NEWS
Mbunge wa Mkuranga,Mhe. Abdallah Ulega,kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM)Mbunge wa Mkuranga, akikata utepe wa uzinduzi wa kisima cha maji katika Shule ya Msingi Lupondo,iliyopo kijiji cha Lupondo kilichojengwa na kwa ufadhiri wa shirika la African Reflection Foundation.
Akizungumza
Mara baada ya kuzindua Kisima hicho, amesema kuwa kijiji cha Lupondo
kilikuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu. Amesema kuwa wananchi hao
walikuwa wakitafuta maji umbali wa kilomita tano na kufanya kuumiza
kichwa katika kuwapata wafadhili wa mradi huo.
Mhe.Abdallah
Ulega amesema katika kipindi cha miezi tisa ameweza kupata miradi ya
maji katika vijiji sita na kuahidi kuendelea kutafuta miradi ya maji
katika vijiji vilivyosalia.Hata hivyo katika uzinduzi huo Mh.Ulega
ametoa msaada wa mifuko 10 ya saruji katika msikiti wa kijiji hicho.
Nae
mratibu wa African Reflection foundation, Shiraz Mohamed, amesema
wataendelea kufadhili miradi ya maji katika vijiji vyenye changamoto
hiyo.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Lupondo jana mkoa wa Pwani
Mbunge
wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Lupondo kabla ya uzinduzi wa kisima cha maji katika kijiji cha Lupondo
jana mkoa wa Pwani.
0 maoni:
Chapisha Maoni