Posted by Esta Malibiche on Oct13.2016 in NEWS
Na Esta Malibiche
Iringa
WAMILIKI wa shule binafsi
na vyuo ukanda wa nyanda za juu kusini Nyasa (TAMONGSCO) wameamua kuunda saccos
yao itakayowasaidia kuendesha shule na vyuo vyao kutokana na
taasisi za kuwapa fedha kwa riba kubwa jambo linalowafanya kujiendesha kwa
hasara.
Wakizungumza na kwenye mkutano
wa drarura wa kupitisha katiba ya saccos hiyo mwenyekiti wa Tamongsco
mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma Lucas Mwakabungu alisema ili kuondokana na
changamoto hiyo wameamua kuanzisha saccos yao itayowasaidia kukopa
fedha za kuendesha shule na vyuo pale wanapokwama.
“Ndugu wanachama saccos yetu hii
ndioyo itakuwa mkombozi wetu kwani kila mmoja wetu hapa anajua adha na karaha
ya tasisi za fedha pindi unapoenda kukopa fedha wanakuwa na masharti magumu na
wakati mwingine kucheleweshewa hela uliyoomba lakni kwa umoja wetu huu
kila mmoja atakuwa ni mmiliki wa saccoso hii na utapata mkopo kwa wakati
muuafaka ’’
Mwakabungu alisema kuwa
kwa kuwa benki zinatoza riba kubwa na upatikanaji wa mikopo inachukua
muda mrefu ndiyo maana wameamua kuanzisha saccos ambayo itawakomboa
kwa kiasi kikubwa na wanategemea ndani ya miezi sita wawe na zaidi ya Mil.500.
Naye katibu wa tomongsco kanda
ya nyasa Nguvu Chengula ambaye ni mmiliki wa shule ya Sun Academy alisema kuwa
shule nyingi zinapofikia mwishoni mwa mwaka zinakumbwa na uhaba mkubwa wa
rasilimali fedha kwa ajili ya kuendesha shule zao na ndio maana wameanzisha
saccos hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwao na riba nafuu tofauti na benki.
Chengula alisema kuwa tasaisi nyingi
za fedha ziwemekuwa zikiwapa masharti magumu yakutaka mtu kuwekeza vitu vya
garama zikiwemo nyumba au gari ili hali muhusika hana vitu kwa kuwa ndio
mchanga katika kuaendesha taasisi za elimu
“Kuna kipindi unaweza kuwa umekwama
na huna fedha za kuendeshea shule na shuleni unawanafunzi wanahitaji chakula na
vitu vingine unaenda kwenye taasisi za fedha lakini unazungushwa wewe mpaka
kuja kupata hiyo fedha na matatizo tayari yamewikisha sasa huo mkopo unatakuwa
na maana gani”
Kwa uapande wake Noah Mtokoma
ambaye ni mwenyekiti wa saccos hiyo ya ukanda wa nyasa alisema kuwa
uaminifu,uadilifu ndicho kitu cha muhimu ambacho kitafanya saccos hiyo kukuwa
kwa haraka
|
0 maoni:
Chapisha Maoni