Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Oktoba 15, 2016 kwa
michezo mitatu ambako Simba inayoongoza katika msimamo wa kuwania taji
hilo katika timu 16 itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja
wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Na.73, mwamuzi
atakuwa Hussein Athuman kutoka mkoani Katavi ambako pembeni atasaidiwa
na Joseph Bulali wa Tanga na Silvester Mwanga wa mkoani Kilimanjaro
wakati Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna
wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati
ya JKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga. Ni mchezo Na. 74 utakaofayika Uwanja
wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambako utachezeshwa na
Mwanamama mwamzi mwenye beji la FIFA, Mwanahamisi Matiku wa Dar es
Salaam, akisaidiwa na Shafii Mohamed pia wa Dar es Salaam na Gesper
Ketto wa Arusha.
Mwamuzi wa akiba atakuwa Abdallah Rashid wa Pwani wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Charles Mchau wa Kilimanjaro.
Pia Stand United ya Shinyanya
itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambarage katika mchezo
Na. 75 ambao utachezeshwa na Eric Onoka wa Arusha akisaidiwa na Agnes
Pantaleo pia wa Arusha na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba
atakuwa Joseph Pombe wa Shinyanga. Kamishna wa mchezo atakuwa Hamisi
Kitila wa Singida.
Ligi hiyo itaendelea keshokutwa
Jumapili kwa mchezo utakaozikutanisha timu za Azam na Young Africans;
zote za Dar es Salaam. Mwamuzi wa mchezo huo Na. 76 atakuwa Israel
Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo atasaidiwa na Soud Lila na Frank
Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar es Salaam.
Mchezo Na. 77 utazikutanisha timu
za Ruvu Shooting na Mbeya City Jumapili Oktoba 16, 2016 kwenye Uwanja
wa Mabatini mkoani Pwani. Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Rudovic Charles
wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jeremina Simon wa
Dar es Salaam. Kamisha wa mchezo huo atakuwa Idelfonce Magali wa
Morogoro.
Mtibwa Sugar ya Morogoro na
Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza Jumapili Oktoba 16 kwenye
Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. Mchezo huo Na. 78 utachezeshwa na
Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi ni Ferdinand Chacha wa
Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa akiba Nicolaus
Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa Dodoma.
Kwa siku ya Jumapili mchezo
mwingine utakuwa ni kati ya Toto African ya Majimaji ya Songea kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mchezo huo Na. 79 utachezeshwa na mwamuzi
Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius
Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa
Mwanza. Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni