Posted by Esta Malibiche on Oct12.2016 in NEWS
Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mkoani
Manyara, Sarah Msafiri Ally akizungumza kwenye uzinduzi wa mfuko wa afya
ya jamii ulioboreshwa (ICHF) wilayani hupo ulioratibiwa na ofisi ya
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara na kufanyika katika
Kata ya Simbay ambapo wananchi wanapaswa kuchangia shilingi 30,000 na
kutibiwa kaya moja yenye watu sita kwa mwaka mmoja.
Mkazi wa Tarafa ya Simbay Wilayani
Hanang’ Mkoani Manyara, Stephan Songay akizungumza kwa kuwasisitizia
wananchi wa eneo hilo kujiunga na mfuko wa afya iliyoboreshwa ICHF kwa
kuchangia shilingi 30,000 na kutibiwa bure kwa mwaka mmoja, kaya moja
yenye watu sita, baba, mama na watoto wanne ambao hawajatimiza umri wa
miaka 18.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Bryceson Kibasa akizungumza na
wananchi wa Tafara ya Simbay kwenye uzinduzi wa mfuko wa afya ya jamii
iliyoboreshwa (ICHF) ambapo alisema wameboresha hospitali ya wilaya hiyo
Tumaini ikiwemo dawa kupatikana kwa wingi.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya
Taifa Nchini (NHIF) Mkoani Manyara, Henry Shekifu akizungumza na
wananchi wa Tarafa ya Simbay Wilayani Hanang’ juu ya umuhimu wa kujiunga
na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (ICHF) ambapo huduma hizo
zitatolewa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali zote za Serikali
ndani ya wilaya pia katika zahanati, vituo vya afya na hospitali
binafsi na taasisi za dini zilizo ndani ya wilaya na kusajiliwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni