Ijumaa, 28 Oktoba 2016

MWIGULU AMREJESHA YANGA KOCHA HANS VAN DER PLUIJM

Posted by Esta Malibiche on Oct 28.2016 in MICHEZO

Mchezaji  wa Mpira wa Miguu namba 11 wa Timu ya Bunge  mashabiki wa Timu ya Yanga,na Mpenzi wa Soka Nchini,Mwigulu Nchemba,amemrejesha kocha wa Timu ya Yanga Hans Van  Der Pluijm ambaye alijiuzulu kuiongoza timu hiyo.
Katika mazungumzo yaliyodumu kwa takribani masaa matatu,na hatimae kufanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani tayari kwa kuendelea na kazi yake ya ukocha.
Mwigulu ambae ni mshabiki wa Timu hiyo na mchezaji  namba 11 wa Timu ya bunge washashabiki wa Timu ya Yanga,hii ni mara ya pili kufanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya club ya Yanga.Msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha kiungo Haruna Niyonzima kuichezea  yanga.
Ikumbukwe kwamba Mwigulu Nchemba ni Mdau wa michezo nchini, mpenzi wa soka na  mwanachama wa Jangwani YANGA



0 maoni:

Chapisha Maoni