Immaculata Makilika- MAELEZO
Moroco ni nchi iliyopo Kaskazini
Magharibi mwa Afrika, ambayo imepakana na bahari za Atlantiki na
Mediteraniani, na upande wa bara imepakana na nchi za Algeria,
Mauritania.mpaka wa kusini unatajwa kuwa Sahara Magharibi.
Nchi ya Moroko inakadiriwa kuwa
na eneo la Km2 446,550, huku sehemu kubwa ikiwa ni jangwa la Sahara na
watu wengi nchini humo huishi kwenye sehemu zilizo na rutuba hasa karibu
na maeneo ya pwani.
Nchi hiyo ina milima inayofunika
eneo kubwa, ikiwemo milima ya Atlas ambayo ipo katikati ya nchi hiyo
kutoka kusini magharibi kuelekea upande wa kaskazini mashariki na mji
mkuu wake ukiwa ni Rabat wenye wakazi milioni 2, aidha mji mkubwa ni
Casablanka.
Nchi ya Moroco ilipata uhuru wake
mwaka 1956 kutoka kwa nchi za Ufaransa na Hispania zilizokuwa
zikiitawala, na kikatiba inaongozwa na Mfalme, kwa sasa inaongozwa na
mfalme anayeitwa Mohammed wa VI, na Waziri Mkuu ni Abdelilah Benkirane.
Watu wa Moroko hutumia lugha
rasmi za kiarabu na kiberiberi. Fedha yao inajulikana kama Dirham,
zaidi ya 90% ya watu wake ni waislamu.
Uchumi wa Moroco unategemea zaidi utalii, sekta ya mawasiliano, viwanda vya nguo pamoja na kilimo.
Hivi karibuni, kwa mara ya
kwanza tunashuhudia ziara ya Mfalme wa Moroco Mohammed wa VI aliyewasili
nchini wiki hii kwa ziara ya siku tatu hadi Oktoba 25 mwaka huu.
Ujio wa Mfalme huyo wa Moroko
unaidhihirishia dunia kwa kiasi gani diplomasia ya Tanzania imeendelea
kukua kwa kasi, ikiwa ni sambamba na kukuza diplomasia ya uchumi.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga anasema kuwa
lengo la ziara hiyo ni kukuza uhusiano wa kati ya Tanzania na Moroco
hususani katika masuala ya uchumi na biashara kwa faida ya watu wa nchi
hizi mbili.
“ Ziara hii imejikita zaidi
katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na biashara, ikizingatiwa kuwa
nchi ya Moroco imefanikiwa katika nyanja mbalimbali kama vile
miundombinu, afya, madini na ulinzi”.
“Vile vile wafanyabiashara
kutoka Moroko watafanya mazungumzo na wa hapa nchini kwa lengo la
kubadilishana uzoefu na ni hatua nzuri itakayoweza itakuza uhusiano wetu
pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi” anasema Balozi Mahiga.
Maroko imepiga hatua katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii, uvuvi ,viwanda, kilimo na madini.
Mambo yaliyopo katika mpango huo
ni pamoja na maboresho ya reli, na barabara, kuboresha viwanja vya ndege
kwa viwango vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya ndege
zinazoingia Moroco. Sambamba na hilo bandari maarufu zimeandaa utaratibu
wa safari za kitalii.
Vitu na Maeneo mbalimbali
yamekuwa sehemu ya kuvutia utalii kutoka nchi za Ujerumani, Ufaransa,
na Hispania, ambapo huvutiwa na fukwe za bahari,milima ya Atlas, pamoja
na miji maarufu ya kama ya Tangie, Marrakech, Casablanka na Tarfaya.
Sekta ya madini ni sekta muhimu
kwa vile inachangia uchumi wa nchi kwa asilimia 6 ya pato la ndani la
taifa na asilimia 35 ya pato la kigeni kwa nchi ya Moroco.
Ili kukuza sekta ya utalii nchini
humo, matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
yameimarishwa na kuweza kutangaza vivutio mbalimbali kwa kuhususha
sekta binafsi katika kutangaza utalii wa ndani, na kati ya nchi
zilizofanikiwa katika hilo ni pamoja na nchi ya Malaysia ambapo mwaka
2011 ilipata watalii milioni 24.7 na mwaka 2012 ilipata watalii milioni
25 kutokana na matumizi ya TEHAMA.
Jitihada mbalimbali zimefanyika
katika kusaidia sekta ya utalii nchini kukua na kuchangia zaidi pato
la taifa, ambapo kupitia maboresho kuongeza ndege zenye safari ya moja
kwa moja hadi nchini, na kuboresha miundombinu ya barabara sekta hiyo
imeweza kupata mafanikio.
0 maoni:
Chapisha Maoni