Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo ameagwa  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  kwa safari yake ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili. Hii ni safari yake rasmi ya tatu kwenda nje ya nchi toka aingie madarakani mwaka mmoja uliopita. Alisafiri kwa mara ya kwanza alikwenda Rwanda, kisha akaenda Uganda.
imgs0002Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa safari hiyo mapema leo
imgs0014Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Balozi wa  Kenya nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili  leo Oktoba 31, 2016
imgs0022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. 
imgs0028 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana  na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa  tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
magufuli kenya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wakati akipanda ndege kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
imgs0038 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akianza  safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. 
PICHA  ZOTE NA IKULU