Posted by Esta Malibiche on Oct 14 .2016 in BURUDANI
Watoto wakichuana kukimbia mbio za mita 50 kwenye Bonanza hilo. |
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice akionyesha umahiri wake kwenye mchezo wa Karate |
Kikundi cha Karate kikonyesha mbinu za mchezo huo |
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha
kwa kushirikiana na wadau wa michezo pamoja na wananchi wa Jiji
wameadhimisha siku ya Mwl. Nyerere kwa kuandaa na kushiriki kwenye
Bonanza la Michezo lililopewa Jina la Bonaza la Mwalimu Nyerere
lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa leo
tarehe 14.10.2016.
Tamasha hili limeandaliwa maalumu
kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyenyere
aliyefariki miaka kumi na saba iliyopita sambamba na kusherekea kilele
cha Mwenge wa Uhuru ambao ulipita katika Wilaya ya Arusha mwishoni mwa
mwezi wa nane na kuzindua miradi ya Afya, Maji, Elimu, Uwezeshaji
wananchi, uwezeshaji makundi maalumu, Ujenzi na Usafi wa Mazingira yenye
thamani ya zaidi ya TshBil 1.5.
Akiongea na wanamichezo
walioshiriki katika Bonanza hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusa Mhe. Gabriel
Fabian Daqarro alisema Tamasha hili ni kwa ajili ya kumuezi Mwl.
Nyenyere ambapo litasaidia vijana na wananchi kuweka miili yao safi,
kujiepusha na maradhi pamoja na makundi yanayoweza kusababisha
kujiingiza kwenye madawa ya kulevya, ulevi na uzururaji.
Pia tuitumie siku hii kutafakari mafundisho na maelekezo ya Mwalimu Nyerere aliyoyatoa wakati wa uhai wake, wapi Nchi imetoka, Misingi imara ya Uongozi bora na namna gani tunaweza kuenenda ili kuleta maendeleo katika Taifa letu, na vijana kama nyie ndio mnaotakiwa kuwa chachu katika kupambana na umasikini katika Nchi yetu alisema Dc Daqarro.
Pia tuitumie siku hii kutafakari mafundisho na maelekezo ya Mwalimu Nyerere aliyoyatoa wakati wa uhai wake, wapi Nchi imetoka, Misingi imara ya Uongozi bora na namna gani tunaweza kuenenda ili kuleta maendeleo katika Taifa letu, na vijana kama nyie ndio mnaotakiwa kuwa chachu katika kupambana na umasikini katika Nchi yetu alisema Dc Daqarro.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya
Arusha Bw. David Mwakiposa alielezea Tamasha hilo kuwa limeshirikisha
michezo mbalimbali kama Netball, Football, Volleyball, Basketball,
mchezo wa Bao, kukimbiza kuku, Baiskel, kuvuta kamba, Karate, Taekondo,
Uchoraji pamoja na riadha.
Bonaza hili pia limetumika kama
jukwaa la kuendelea kuelimisha na kueneza ujumbe kwa vijana kupitia
kauli mbiu ya Mwenge mwaka 2016 inayosema “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa
washirikishwe na wawezeshwe”.
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha
14.10.2016
0 maoni:
Chapisha Maoni