Posted by Esta Malibiche On Oct12.2016 in KITAIFA
Na Esta Malibiche
Iringa
MGANGA
Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari amewataka
watumishi na Afya Nchini kuendelea
kuwaudumia wananchi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao ili wagonjwa wanaofika Hospitalini waweze kupata matibabu yaliyo bora.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya katika uzinduzi wa mradi wa jengo la upasuaji na
kituo cha kutolea damu katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa,iliyojengwa
kwa ufadhiri wa Hospital ya Vicenza kutoka Italia pamoja nakampuni ya Asas iliyoko mkoani
Iringa,Prof.Muhamad alisema kuwa njia
bora ya kulipa fadhira kwa wafadhiri waliojitolea kujenga ni kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora zaidi na
stahiki ili kuwatia moyo wahisani na hatimae kuendelea kutoa misaada mingi na mikubwa zaidi.
‘’’’’’’Sera ya Serikali ni kuhakikisha inashirikiana kwa ukaribu na
wadau mbali mbali wa maendeleo zikiwemo Taasisi na Mashirika ya kidini na Taasisi na mashirika ya Kimataifa,
katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini. Hivyo napenda
kuchukua nafasi hii kuupongeza sana Uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa jitihada walizofanya
ili kulifanikisha jambo hili la ushirikishwaji wa wadau. Haya tunayoyashuhudia
leo hii yasingewezekana kamwe kama hali ingekuwa vinginevyo. Hivyo naomba
kuwatia moyo muendelee na jitihada hizi za kushirikisha wadau na wananchi kwa
ujumla katika utatuzi wa changamoto za kiafya zilizopo.’’’’’’’’alisema
Prof.Muhamad
Prof.Muhamad alisema kuwa, miongoni mwa Malengo endelevu ya Serikali ya
awamu ya tano ni kuhakikisha inapunguza vifo vya akina mama wakati wa uzazi na
vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. Pia malengo hayo, yametafsiriwa
na kueendana sambamba na Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi, (MMAM]
.
‘’’’’’’Natambua kuwa tunazo changamoto
nyingi katika kufikia malengo yetu, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na wataalamu wa
kutosha na wa fani zote muhimu katika utoaji wa huduma za Afya. Tafiti
mbalimbali zinaonesha kuwa watumishi waliopo kazini ni asilimia 51tu ya
mahitaji yote ya watumishi wa sekta ya Afya. Upungufu huu umeathiri zaidi
taaluma nyeti, ikiwemo taaluma ya huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU) na wale wa
nusu kaputi (Anaesthesiologists). Ili kutatua changamoto hii, Serikali
itaendelea kutoa kipaumbele katika kufundisha na kuajiri wataalam wa Afya, hasa
wa fani zenye upungufu mkubwa, na vile vile kutoa kipaumbele cha kuwapeleka
Watumishi wanaojiriwa katika maeneo yenye upungufu mkubwa zaidi, ili kuboresha
huduma kulingana na uwezo wa bajeti. Aidha, kwa vile mchakato wa ajira za
Watumishi unaanzia katika Halmashauri na Mikoa kwa kuweka mahitaji hayo katika
bajeti, hususani ya hospitali, napenda niwasisitizie kuwa wakati wa upangaji wa
bajeti mzingatie mahitaji yenu ikiwa ni pamoja na wataalamu wa huduma za
wagonjwa mahututi na nusu kaputi’’’’’’Alisema Prof.Muhamad
‘’’’’Kama mnavyofahamu, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais
– Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) hupanga wataalamu
kulingana na mahitaji na idadi ya nafasi tunazopewa. Hivi sasa mnatambua kuwa
ajira zimesitishwa, hivyo pindi ruhusa ya kuajiri itakapotolewa mtapatiwa hao
wataalamu kadri itakavyokubalika..Kwa wataalam wetu nawapongeza kwa kufanya
kazi kwa kujituma, hata katika uchache wenu, na katika mazingira yenye
mapungufu mengi. Nitoe rai tena kuwa muendelee kuwahudumia wananchi kwa moyo
wote, na kwa kuzingatia maadili na weledi wa Taaluma zenu’’’’’’’Alisema
Prof.Mahamud
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Robert
Salimu akisoma taarifa ya miradi hiyo alisema, kuwa miradi hiyo itasaidia kuboresha
utoaji wa huduma za upasuaji mdogo na
mkubwa kutokana na eneo kubwa la
kufanyia kazi,Kuzuia magonjwa ya kuambukiza kati ya wagonjwa,Kupunguza vifo
vinavyotokana na upasuaji,Kupunguza gharama za Rufaa, kufuata huduma za
kibingwa Hospitali ya Muhimbili na Hospitali za Kanda,Kuongeza nafasi kwa
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Tiba kujifunza pamoja na Kuwavutia madaktari bingwa
kutoka Hospitali ya Taifa na Kanda kuja kufanya upasuaji katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa
Dkt
Robert aliongeza kuwa moja ya changamoto inayoikabili Hospitali hiyo nipamoja
na kutokuwepo kwa wataalamu wa kutoa dawa ya usingizi (Anaethetist) katika
Hospitali hiyo,hivyo aliiomba Serikali
iweze kusaidia kutatua changamoto hiyo.
Awali Mganga
mkuu mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Maseleta Nyakiroto akisoma
taarifa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa alisema kuwa ,Hospitali
hiyo inakabiliwa na changamoto ni uchakavu wa gari la kubebea wagonjwa
[Ambulance] inayopelekea kuharibika mara kwa mara na kusababishia gharama kubwa
za matengenezo na kuleta usumbufu kwa
wagonjwa pindi wapatapo refaa.
‘’’’’Hospitali hii inakabiliwa na uhaba wa watumishi
hasa madaktari bingwa,Maafisa wauguzi,na wataalamu wengine.Pia idara ambazo
hazina madaktari bingwa hivi sasa zinasimamiwa na madaktari wa
kawaida,hali hii inaathiri utoaji wa
huduma bora kwa wagonjwa’’’’’ alisema
Nyakiroto
Nyakiroto alisema kuwa changamoto nyingine
inayowakabili ni ufinyu wa bajeti
inayotengwa kwa matumizi ya kawaida[OC] na kwa ajili ya kununua dawa na vifaa
tiba kupitia MSD.Kutosekana kwa baadhi ya dawa muhimu na vifaa tiba mara kwa
mara bohari ya dawa ya kanda
‘’’’’’Mheshimiwa Waziri tunakabiliwa na uhaba wa
nyumba za watumishi hasa madaktari na madaktari bingwa.Pia tuna ukosefu wa wa
kitengo muhimu kama vile kitengo cha kuhudumia
wagonjwa mahututi [ICU] na kitengo cha huduma ya dharura
[Casualty/Emegency Unit]’’’’alisema Nyakiroto
MWISHO
Askofu wa jimbo katoliki la Iringa Tarcisius Ngalalekumtwa ambae ni Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania kushoto kwake ni Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Robert Salim
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakisikiliza kwa makini
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakisikiliza kwa makini |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Robert Salim akisoma Taarifa ya Miradi ya M,aendeleo iliyozinduliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Ahammad Bakari
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu akizungumza
Mganga Mkuu wa Seriokali Prof.Muhammad Bakari akitoa Hotuba yake katika,katika uzinduzi huo
Mganga Mkuu wa Seriokali Prof.Muhammad Bakari akiendelea kuzungumza
Mganga Mkuu wa Serikali Muhamad Bakari akikagua chumba cha upasuaji
Mganga Mkuu wa Serikali Muhamad Bakari akikagua na kupokea maelezo katika chumba cha upasuaji
Mhashamu baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa Tarcisius Ngalalekumtwa ambae pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzazia akishangiliwa na watumishi wa Hospitali hiyo na kupongezwa kwa kuleta wafadhiri waliojitolea katika ujenzi wa jengo hilo
Mganga Mkuu wa Serikali Pro.Muhammad Bakari,Katibu Tawala wa Mkoa wa Irina Wamoja Ayubyu Pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Robert Salim wakielekea katika jengo la kuchangia damu salama
Mganga mkuu wa Serikali Prof.Muhmmad Bakari akisalimiana na wafanyakazi katika kituo cha damu salama kilichojengwa na Kampuni ya Assas
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Muhammad Bakari akizindua kituo cha Damu salama kilichojengwa na Kampuni ya Assas
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Muhammad akikagua kituo cha Damu salama kilichojengwa na Kampuni ya Asas baa ya uzinduzi.Picha na Esta Malibiche[ KALI YA HABARI BLOG]
0 maoni:
Chapisha Maoni