Jumatatu, 10 Oktoba 2016

WAZIRI MWIGULU ALA KIAPO CHA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA


c1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Ferdinand Wambali (katikati) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Eva Nkya.
c2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Ferdinand Wambali (katikati) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Eva Nkya.
c3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba (kulia) akipokea hati ya kiapo kutoka kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Ferdinand Wambali mara baada ya Waziri huyo kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

0 maoni:

Chapisha Maoni