Posted by Esta Malibiche on Oct17.2016 in BIASHARA
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa
Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa
wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka
2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Baadhi ya wawakilishi kutoka
taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji
viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa
uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo
Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (katikati) akifuatilia mada mbalimbali
zilizowasilishwa na wadau mbalimbali wakati uzinduzi wa matokeo ya sensa
ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar
es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa
ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es
Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa
maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi wa
matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17,
2016 Jijjini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa
Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa
wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka
2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu mbalimnbali vya
taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya
mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto) akimkabidhi taarifa ya kitabu
cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka
2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo Oktoba 17, 2016
Jijjini Dar es Salaam
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
……………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo
MAELEZO-Dar es Salaam
SERIKALI imeitaka Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo
Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda
Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili kubaini idadi na maendeleo
ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini NA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati wa
uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.
Dkt Mwijage alisema kuwa katika
mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na
Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi
kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.
Alisema katika kuharakisha kasi
ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake imekusudia
kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo vidogo na
vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia kuinua
uchumi wan chi.
“Asilimia 25- 40 ya mazao ya
kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika
kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo
vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi
mazao yao” alisema Mwijage.
Aidha, Dkt Mwijage alisema, sekta
ya viwanda vidogo vidogo nchini imeendelea kukua kwa kasi nchini ambapo
hadi sasa kuna jumla ya viwanda 3800 vilivyoanzishwa nchini kuanzia
Novemba 2015 hadi octoba, 2016.
Katika hatua hiyo Dkt Mwijage
alisema kuwa Wizara yake inaendelea kuhamasisha Sekta binafsi kuwekeza
katika Sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ikiwa jukumu kuu la
Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na inajenga mazingira
wezeshi kwenye sekta binafsi kuzalisha na kufanya biashara.
Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alisema kuwa matokeo hayo
yanaonyesha mafanikio katika sekta ya viwanda ikiwemo kuongezeka kwa
ajira zipatazo 264,223 nchini na kuchangia uchumi kwa takribani Shilingi
bilioni 8.0 kwa mwaka 2013.
Alisema kuwa Takwimu za matokeo
ya sense ya uzalishaji viwandani ni rasmi na kuwataka watunga sera,
wanasiasa, viongozi, sekta binafsi na watu binafsi kutumia matokeo hayo
kwa lengo la kuboresha Sekta ya viwanda nchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni