Ijumaa, 28 Oktoba 2016

MKUU WA MKOA WA IRINGA AMINA MASENZA AFANYA ZIARA KUKAGUA UJENZI HOLELA,USAFI WA MAZINGIRA NA KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHOO BORA

Posted by Esta Malibiche on Oct 28. 2016 in NEWS


 
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza,Katibu tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu Pamoja na Katibu Tawala wa Iringa Joseph Chitinka wakisoma Taarifa ya fupi ya mkakati wa kuboresha vyoo na Usafi wa Mazingira kwa ujumla
 
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akikagua maeneo yaliyojengwa holela katika kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa,ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Iringa akikagua ujenzi holela,Usafi wa Mazingira pamoja na kuhamasisha wananchi kujenga choo bora.
 Viongozi wa serikali za mitaa katika kata ya Kitwiru wakimsikiliza mkuu wa mkoa [hayupo pichani] wakati akizungumza kabla ya kuanza kukagua maeneo yaliyojengwa kiholela katika kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa  katika  ziara yake aliyoifanya jana.

 Afisa mtendaji wa kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa akimuonyesha mkuu wa mkoa maeneo yaliyojengwa kiholela bila kufuata utaratibu.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza baada ya kutembelea na kukagua maeneo yaliyojengwa holela katika kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa


Na Esta Malibiche
Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Msenza amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa kuwa waadilifu na kutojiingiza  katika mauzo ya Ardhi ili kuepuka Migogoro ya Ardhi.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na viongozi wa kata ya Kitwiru iliyopo Manispaa ya Iringa katika ziara yake aliyoifanya janahuku akiambatana na  katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu,Watalaam wa Afya na Mazingira kutoka mkoani na Manispaa ya Iringa.
 Masenza alisemakuwa lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua ujenzi holela katika Mtaa wa Kibwabwa’ B’,kukagua  uchimbaji n a upondaji wa mawe unaofanywa na baadhi ya wananchi  katika eneo la shule ya Msingi Mnazi mmojapamoja na Kukagua hali ya usafi wa Mazingira katika mtaa wa Kitwiru na Uyole .
‘’’’Ninatoa agizo kwa wale wote wanaoporomosha mawe na kujenga naomba wachukuliwe hatua za kinidhamu.Milimani,Mabondeni na katika vyanzo vya uhifadhi hairuhusiwi kujengwa,ninawaomba Manispaa iweke vibao vitakavyoonyesha maeneo yaliyohifadhiwa ili  yasivamiwe na kuuzwa’’’’alisema Masenza
Aliwasihi wananchi kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kupata vibari vya ujenzi na mara wanapotaka kununua uwajanja na kujenga nyumba ili kuepukana na Migogoro ya udanganyifu kutoka kwa viongozi wasio waaminifu.
‘’’’Wenyeviti wa mitaa tuendelee kutoruhusu wananchi wasitende makosa ya kujenga bila kufuata kanuni na taratibu za ujenzi ikiwa ni pamoja na kufuata michoro iliyopo’’’’’’alisema Masenza
Awali kaimu Mkurungenzi wa Manispaa ya Iringa Omary Mkangama,akisoma Taarufa ya kuzuia ujenzi holela,Mikakati ya kulasimisha makazi,kuzuwia uvamizi katika maeneo ya milimani  na uasafi wa Mazingira kwa mkuu wa mkoa  wa Iringa,alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni miongoni mwa    Halmashauri zinazokuwa kwa kasi kubwa hivyo kupelekea tatizo la ujenzi holela kukithiri katika maeneo yasiyopimwa na uvamizi katika maeneo ya mlimani.
Mkangama alisema hali hiyo inatokana na ongezeko la idadi ya watu,kutanuka kwa mji na ufinyu wa maeneo yaliyopimwa.Pia maeneo yaliyokithiri kwa ujenzi holela  ndani ya Manispaa hiyo ni pamoja na Ipogolo,Mapogolo,Ndiuka,Semtema,Mtwivila,,Mwangata,Mlandege,Igumbilo,Kihondombi,Isoka,Mafifi,na milima ya Mkimbizi.
‘’’’Mikakati mbalimbali tumeiweka ili kuzuwia ujenzi holela  na uvamizi wa  maeneo yasiyopimwa ikiwa ni pamoja na kutumia makampuni ya wapima binafsi kupima viwanja kwenye maeneo yenye michoro ya mipango miji kwa gharama zilizotolewa na Serikali.
Alisema  wanaendelea kutoa vibali vya ujenzi kwa haraka hasa kwenye maeneo yaliyopimwa ili kuepuka wananchi kujenga pasipo kufuata taratibu.Kuendelea kuuza viwanja vilivyopimwa kwa kuzingatia pato la mwananchi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Kitwiru Simba Nyunza akisoma  Taarifa ya mikakati ya uboreshaji wa matumizi ya vyoo bora na Usafi wa mazingira kwa ujumla alisema kuwa majengo 2255 ndiyo yenye vyoo bora sawa na asilimia 93 ya majengo yote yaliyotambuliwa.
Nyunza alisema kuwa mikakati ya kata ni kuondoa na kuwezesha idadi ya majengo 168 yenye vyoo vinavyohitajika kuboreshwa viboreshwe mpaka kufikia mwisho wa mwezi Novemba mwa huu 2016.Na kwa wale watakaobainika kushindwa kutekeleza agizo hilo sheria ndogo ya Halmshauri itatumika.
‘’’’’’Baadhi ya wakzi wanashindwa kujenga vyoo bora kwa kuwa maeneo yao yana Ardhi oevu,hivyo wanashindwa kuchimba mashimo kwa kuwa maji chini ya Ardhi yapo jirani sana.Pia Ardhi iliyopo ni ya mchanga sana.Hivyo tunashirikisha wataalamu wa ziada kutoka ofisi ya Afya ya Manispaa kutoa Elimu ya Ujenzi wa vyoo bora katika maeneo oevu.’’’’’’alisema Nyunza
Akielezea mikakati ya kutdhibiti ujenzi holela alisema ili kudhibiti ujenzi holela, kamati za mitaa ambazo ni kamati za mazingira ambazo ziliagizwa kufuatilia vibali vya ujenzi na kutoa maelezo ya namna ya kuomba vibari vya ujenzi kwa wajenzi wote kila mtaa ujenzi unapotokea.



0 maoni:

Chapisha Maoni