Posted by Esta Malibiche
on
News
Mfanyabiashara
Julius Masalu (58) mkazi wa Mwanza ameibuka mshidi wa gari aina ya
Eicher lenye thamani ya shilingi milioni 56 katika mzunguko wa pili wa
bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi
iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers
Ltd (TDL).
Droo
ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika katika viwanja vya hoteli ya Kili
Home mjini Moshi mwihoni mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa
ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa na kusimamiwa na afisa wa Bodi ya
Taifa ya michezo ya kubahatisha Humudi Abdul Hussein.
Akiongea
kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Masalu alisema ametoka
Mwanza akiamini kuwa atajishindia gari hilo na kwamba bahati nasibu hiyo
imeendeshwa kwa uwazi na hakuna upendeleo unaoweza kufanyika.
Mfanyabiashara Julius Masalu
mkazi wa Mwanza (katikati) akipokea funguo za gari alilojishindia
katika droo ya promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha
mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL)
kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Konyagi,Martha Bangu (Kulia). Droo ya pili
ya promosheni hiyo ilifanyika mwishoni
mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwishoni
mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na
kanda ya ziwa.
“Katika
bahati nasibu hii hakuna longo longo,shindano limeendeshwa kwa uwazi
mkubwa sana na namshukuru Mungu kwa kuweza kupata zawadi hii ya gari
itanisaidia sana katika kusambaza bidhaa za kampuni ya konyagi kwa
wateja wangu,” alisema Masalu.
Kaimu
Meneja Mkuu wa Konyagi, Devis Deogratius alisema dhumuni ya
promosheni hiyo ni kukuza uhusiano wa kibiashara na wasambazaji wa
bidhaa za TDL pamoja na kuwapatia kifaa kitakachosaidia katika kupanua
masoko ,kusambaza na kuongeza ufanisi.
“Safari
ilianza mwezi wa saba hadi mwezi wa tisa ,kumekuwa na usawa katika
mchakato huu wa kumpata mshindi na hakuna upendeleo wowote ,wale ambao
wamefikia malengo wamefika katika promosheni hii na kuwepo hali ya
usawa katika kushinda zawadi ya gari”alisema Deogratius.Alisema mbali na
mshindi huyo wa gari katika droo hii ya kwanza washiriki watano
walibahatika kujishindia katoni 10 za Konyagi kila mmoja.
Mawakala wa Konyagi wakiserebuka wakati wa hafla hiyo.
Baadhi
ya washiriki katika droo hiyo, Mkamba Zephania na Joas Muganyizi
walisema wameridhishwa na mchakato mzima ulivyofanyika katika kuchezesha
droo na wala hapakuwa na kasoro ama udanganyifu wowote.
“Kampuni
ya TDL kupitia bidhaa yake ya Konyagi katika promosheni ya Nunua
Uza,Shinda na Konyagi imesaidia kuwakutanisha wafanyabiashara wa maeneo
mengine ya kanda ya Kaskazini na kanda ya ziwa hali inayochangia
kuongeza wigo katika kufanya biashara”.Alisema Muganyizi.
Washindi
wengine waliojinyakulia katoni 10 kila mmoja za bidhaa ya Konyagi na
maeneo wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Linus Mathew (Kagera) Msemo
Enterprises (Arusha) ,Joace Muganyizi(Bukoba) Mkamba Zephania (Bariadi)
na Yohana Masunga (Geita).
Huu
ni mzunguko wa pili wa droo ya bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua
Uza,shinda na Konyagi ambapo katika droo ya kwanza mfanyabiashara Grace
Oroki, mkazi wa Jijini Dar es salaam, alijinyakulia gari kwa mawakala
wa kuuza bidhaa za kampuni ya TDL wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini na
Pwani.
Meneja Masoko wa TDL,George Kavishe akiwashukuru mawakala walioshiriki kwenye promosheni hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Devis Deogratius akiongea na mawakala na wageni waalikwa.
Baadhi ya maofisa wa TDL na mawakala katika picha ya pamoja.
0 maoni:
Chapisha Maoni