Posted by Esta Malibiche on Oct13.2016 in NEWS
Afisa wa Uthibiti wa Majaribio na
Usalama wa Dawa (TFDA)Dkt. Alex Nkayamba kushoto akimpa maelekezo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
kuhusu mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa
unavyopatikana kwenye simu za mkononi wakati wa hafla yauzinduzi wa
huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu
wa TFDA Bw. Hiiti Sillo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akiangalia
jinsi mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa
unavyofanya kazi katika kutoa tarifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa
huduma hiyo, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti
Sillo.
Wadau mbalimbali wa vyakula na
dawa wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa
uzinduzi wa mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya
dawa uliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………
Na Ally Daud-MAELEZO
WANANCHI waaswa kutoa taarifa
pale wanapohisi wamepata madhara ya dawa wanazozitumia ili kuirahisishia
Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuchukua hatua
stahiki zidi ya watengenezaji wa dawa hizo ili zisiendelee kuwadhuru
wananchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwenye hafla ya
uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya
dawa uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri Ummy amesema kuwa wananchi
wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa pindi wanapohisi kupatwa na
madhara ya dawa wanazozitumia ili kuirahishia TFDA kuchukua hatua
stahiki kutokana na taratibu na sheria zilizopo za kuondoa madawa feki
nchini.
“Napenda kusisitiza kwa wananchi
wote kutoa taarifa pale wanapohisi wamepata madhara ya dawa ili
kuirahishia TFDA kuchukua hatua stahiki kutokana na utaratibu na sheria
zilizowekwa” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
bila taarifa hizi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kupitia TFDA itashindwa kuchukua hatua muafaka na za haraka
katika kudhibiti madhara yanayotokana na matumizi ya dawa na hivyo
kuendelea kusababisha athari kwa watumiaji.
Waziri Ummy amesema kuwa wataalam
wa afya na wananchi wote kwa ujumla wanatakiwa kutoa taarifa za
madhara ya dawa kwa wakati, kwa wale wenye simu zilizounganishwa kwenye
“internet” watumie simu hizo kutoa taarifa za madhara ya dawa, na wale
wenye kompyuta zilizounganishwa kwenye “internet” watumie kompyuta hizo
na wale wasio na simu wala kompyuta zilizounganishwa kwenye “internet
“waendelee kutoa taarifa kwa kutumia fomu za njano na kijani.
Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa
TFDA Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa ujazaji wa taarifa hizo kwa kutumia
njia za kielektroniki kunasaidia kujua dawa zipi ni sahihi na zipi si
sahihi kwa matumizi ya binadamu na hivyo kuchukua hatua inayostahili.
“Napenda kuwaambia wananchi
wajaze fomu hizo ili kutoa taarifa za madhara ya dawa wanazozitumia ili
kufahamu dawa zipi ni sahihi kwa matumizi ya binadamu na kama sio sahihi
basi tuzichukulie hatua zinazostahili” alisema Bw. Sillo.
Aidha Bw. Sillo amesema kuwa moja
ya hatua ambayo zitachukuliwa pindi taarifa za madhara ya dawa
zinapotolewa ni kufungia kiwanda kinachotengeneza aina hiyo ya dawa au
kusimamisha matumizi yake ili kuondoa dawa zinazoleta madhara kwa
watanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni