Posted by Esta Malibiche on Oct13.2016 in NEWS
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa
mkoa mara baada ya kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi
ya kutembelea vituo vya kulea wazee na watu wasiojiweza vya Chazi na
Fungafunga vyote vilivyopo Mkoani huko.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa
mkoa mara baada ya kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi
ya kutembelea vituo vya kulea wazee na watu wasiojiweza vya Chazi na
Fungafunga vyote vilivyopo Mkoani huko.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni Ikulu Ndogo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Viongozi wa makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo
Manispaa ya Morogoro wakimuonesha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
waTanzania Mama Janeth Magufuli maeneo ya miradi yaliyokatika makazi
hayo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee wanaoishi
katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya
Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee wanaoishi
katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya
Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma ya asili na
baadhi ya viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji
maalum ya Fungafunga
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar
akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth
Magufuli hotuba.
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na Wazee katika makazi
ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo
Manispaa ya Morogoro ambapo amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali
Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa
maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye
ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa
kadri iwekenavyo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi ya Chakula
Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji
maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki.
Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph
Kaniki. Akimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa msaada wa chakula na
kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo kwani kusaidia wazee ni
kulisaidia taifa pia.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya kuku kutoka
kwa mmoja wa kiongozi wa makazi ya wazee ya Fungafunga.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya
Fungafunga
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwaaga baadhi ya Wazee na
watu wenye mahitaji maalum katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye
mahitaji maalum ya Fungafunga
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
……………………………………………………
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Wizara, Taasisi za Serikali
Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa
maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye
ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa
kadri iwekenavyo.
Hayo yamesemwa na Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu wenye ulemavu
alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha
Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.
“Kundi hili ni moja kati ya
makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi kikubwa ni kundi
ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa mahitaji muhimu
wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za Serikali
Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa
maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili
kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama
Janeth.
Pia Mama Janeth alisema kuwa
serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika kukuza uchumi
wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali
katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote
muhimu.
Aidha, Akiongea wakati wa
kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari Kilo 175,
Maharage Kilo 350 na Mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama
Janeth aliwataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha chakula hicho
kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa.
Akiongea wakati akimkaribisha
Mama Janeth Magufuli, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Regina Chonjo
aliwataka ameataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa mara na
viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa
changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.
Naye Kaimu Afisa Mfawidhi wa
Kituo hicho Bw.Rashid Omar alimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa uamuzi
wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa wazee na watu
wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.
0 maoni:
Chapisha Maoni