Posted by Esta Malibiche on Oct 28.2016 inNEWS
Dkt. Bernard Achiula:
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Udhibiti wa huduma ya habari kwa
namna ya ili kulinda usalama, utulivu amani na maslahi ya kiuchumi,
maadili au afya ya jamii ni jambo jema ambalo huzingatiwa na nchi zote
duniani.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa
Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Achiula alipokuwa akifanya mahojiano
kuhusu namna muswada sheria ya huduma za habari unavyoweza kusaidia
kukuza diplomasia ya uchumi nchini.
Dkt. Achiula alisema kuwa vyombo
vya habari vina jukumu kubwa la kulinda amani ya nchi na kwa kuwekwa
misingi ya uwajibikaji kwa waandishi wa habari itakayosaidia kulinda
maslahi ya Taifa.
“Muswada huu upitishwe ili vyombo
vya habari vifanyekazi katika misingi ya taaluma kwa kutoa taarifa
zenye kweli kwa jamii, zitakazoitangaza nchi kimataifa ili kujenga
diplomasia ya uchumi, itakayosaidia katika kulinda heshima utulivu na
amani ya nchi”
“Muswada huu pia utasaidia
waandishi wa habari kuandika habari zitakazoiletea sifa nchi na kuvutia
watalii na wawekezaji kwa kuzingatia amani iliyopo nchini, mbali na
hapo diplomasia ya uchumi itaweka mazingira rafiki katika kufikia azma
ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya kufikia uchumi wa kati
kupitia viwanda ifikapo mwaka 2020” alisema Dkt. Achiula
Sehemu hii ya muswada wa huduma za
habari unaakisi mikataba ya kimataifa ikiwemo mkataba wa geneva ibara
ya 19 inayoainisha haki wa wajibu kwa mwandishi wa habari hasa katika
maeneo yanayohusu usalama, utulivu amani na maslahi ya kiuchumi, maadili
au afya ya jamii.
Akizungumzia kuhusu Bodi ya
Ithibati iliyopo katika muswada huo, Dkt. Achiula alisema kuwa Bodi hiyo
itasaidia kukuza kanuni za maadili kwa wanahabari na kukuza weledi
jambo litachochea mahusiano yenye faida katika nyanja za kimataifa.
Ameongeza kuwa kuwemo kwa Baraza
Huru la Habari kutasaidia kuijengea uwezo sekta habari nchini kwa vile
muswada huo utazalisha waandishi wa habari waliobobea katika fani
mbalimbali, huku akitolea mfano nchi zilizoendelea ikiwemo Ujerumani kwa
kuwa na chombo kinachosimamia masuala ya sekta ya habari kwa kufuata
misingi na utaratibu maalumu.
Aidha, wadau wa sekta ya habari
nchini, wametakiwa kuendelea kutoa maoni yao ya kuboresha Muswada wa
huduma za habari, kabla muswada huo kusomwa tena bungeni ifikapo
novemba mosi, mwaka huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni