Posted by Esta Malibiche on Oct9.2016 in KITAIFA with No Comment
Waziri
wa Habari, Sanaa na Michezo Nane Nnauye akitoa hotuba ya kufunga
Tamasha la Ngoma za Asili lililoandaliwa na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amefunga Tamasha la
shindano la Nyimbo za Jadi Rungwe na kuonesha kufarijika na mwitikio
mkubwa.Tamasha
hilo ambalo lilifanyika kwa siku mbili kati ya Oktoba 7 na 8 mwaka huu
likihusisha halmashauri tatu za Kyela, Rungwe na Busokelo.
Waziri
Nape alisema mahudhurio na mwitikio wa tamasha hilo umeimsha Serikali
hivyo kuona ni vema kila Wilaya na Mkoa kufanya matamasha kama hayo hadi
kufikia ngazi ya Taifa.
Aidha
alienda mbali zaidi na kupendekeza uwanja wa Tandale ulipo Tukuyu mjini
ambao ulitumika kwa ajili ya Tamasha kubadilishwa jina na Kuitwa Dk.
Tulia jambo ambalo liliungwa mkona na wananchi zaidi ya 10,000
waliohudhuria.
Alisema
washindi katika matamasha hayo watasaidia kutangaza mila na desturi za
Watanzania, vivutio vya utalii vinavyopatikana nchiniikiwa ni pamoja na
kutengeneza fursa ya ajira kwa vijana.
Kwa
upande wake Dk. Tulia alisema katika Tamasha hilo Vijana 20
watasomeshwa katika Chuo cha Sanaa bagamoyo kwa ngazi ya awali ya miezi
miwili huku vijana 5 watachaguliwa kwenda kusomea cheti ambao watakuwa
wana elimu ya kidato cha nne huku vijana wawili waliohitimu kidato cha
sita wakisomea ngazi ya diploma.
Kwa
upande wao majaji wa Tamasha hilo wakiongozwa na Ismail Michuzi
Mwasulimo waliwataja washindi wa tamasha hilo kuwa ni upande wa Ling’oma
na zawadi zao kwenye mabano kuwa ni Mbagamoyo kutoka Kyela msindi wa
kwanza (750,000), mshindi wa pili Lupaso (500,000) na mshindi wa tatu ni
Njisi (350,000).
Ngoma
ya pili ni Ling’oma aina ya kituli mshindi wa kwanza Kasanga(750,000),
mbamila na Mshindi wa tatu ni Kakindu.(zawadi zote ni sawa kwa kila aina
ya ngoma kwa mshindi wa kwanza 750,000, pili 500,000 na tatu ni
350,000).
Upande
wa Samba ulichukuliwa na Mshindi wa kwanza Katumba, Pili Mpunguti na
tatu Sumu ya Mamba huku maghosi mshindi wa kwanza akiwa ni Kyatasumo,
pili Ilopa na tatu ni Songela.
Ngoma
ya Ndingara mshindi wa kwanza ni Lukwego, pili Mwambula na tatu ni
Itagata huku ngoma ya kitumbwike ikiwa na mshiriki mmoja ambaye ni
Ndobho aliyepata shilingi 350,000.
Kwa
upande wa Lipenenga mshindi wa kwanza ni Iponjola, pili Bugoba na tatu
ni Ipuguso huku upande wa Kibhota akiwa mshiriki mmoja ambaye pia ni
Iponjola aliyepata 350,000.
Ngoma
ya Kapote washindi ni kwanza Usweghe Mwambapa, pili Asamisye na tatu ni
Mwandulusya huku ngoma ya Kimwenge akiwa mshiriki mmoja ambaye ni
Balenga Balandani waliojipatia shilingi 350,000.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitoa salam za Mkoa wa Mbeya wakati wa kufunga Tamasha la ngoma za jadi RungweNaibu
Spika Dk. Tulia Ackson akizungumza jambo kuhusiana na dhamira yake ya
kufufua utamaduni wa Wanyakyusa katika tamasha aliloliandaa RungweMkuu wa Mkoa wa Mbeya akimpongeza Dk. TuliaNaibu Spika Akizungumza jambo na Waziri Nape pamoja na Mkuu wa Mkoa wa MbeyaWaziri
Nape akisalimiana na Mwakilishi waUbalozi wa Ujerumani hapa nchini
baada ya kuwasili katika tamasha la ngoma za Jadi RungweBaadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Mbeya wakiserebuka moja ya ngoma za jadi pamoja na Naibu SpikaNgoma aina ya Ling’oma ikionesha makeke yakeMaelfu ya Wananchi waliojitokeza kushuhudia tamasha la ngoma za jadiNgoma ya kikundi cha Nyati iliyoalikwa kutoka Dodoma ikitoa burudaniWachezaji wa Ling’oma wakionesha umahiri wa kuchezaWaziri Nape akicheza sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pamoja na Naibu SpikaNaibu Spika na Waziri Nape wakicheza ngoma aina ya LipenengaWananchi wakifuatilia kinachoendelea katika uwanja wa TandaleWaziri Nape akitoa zawadi kwa mshindi wa ngomaWaziri Nape akiongoza Wabunge kucheza Kwaito
0 maoni:
Chapisha Maoni