Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa
akisalimiana na Ahmed Olotu(Mzee Chilo) mara baada ya kupokea shilingi
laki sita na ishirini kutoka kwa Mtandao wa wasanii(SHIWATA) ikiwa ni
msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.Wengine
pichani ni Mkurugenzi Idara ya uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Brigedia Gen.Mbazi Msuya na Caasim Taalib(wa tano kushoto) ambaye ni
Mwenyekiti wa mtandao wa wasanii.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ndogondogo solo la
kariakoo mara baada ya kupokea msaada wa nguo mchanganyiko,midoli na
kanzu wenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni msaada wa kusaidia
waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
……………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amepokea fedha taslimu sh. milioni 25.62 pamoja na nguo zenye thamani ya
sh. milioni mbili kutoka kwa wadau mbalimbali.
Makabidhiano ya michango hiyo
yamefanyika leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Akiwashukuru wadau hao Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Nawashukuru kwa kuamua kutumia
siku ya leo ya kukumbuku ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius
Nyerere kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa,” amesema.
Waziri Mkuu amesema michango hiyo ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo baina ya Watanzania.
Misaada hiyo imetolewa na Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO) sh. milioni 20, Mtandao wa Wasanii
Tanzania sh. 620,000 na nguo mifuko miwili, Chama cha Makatibu Mahsusi
(TAPSEA) sh. milioni tano.
Wengine ni Umoja wa
Wafanyabiashara Ndogondogo soko la Kariakoo ambao wametoa marobota
mawili ya nguo (suruali, kanzu na nguo za akinamama na moja la
wanasesere kwa ajili ya watoto waliopatwa na maafa vyote vikiwa na
thamani ya sh. milioni mbili.
Fedha na nguo hizo vimetolewa kwa
ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea
mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya
watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.
Pia tetemeko hilo limesababisha
nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi
na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji
misaada mbalimbali .
0 maoni:
Chapisha Maoni