Posted by Esta Malibiche on Oct 31.2016 in NEWS
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya
Mawasiliano Serikalini (GCU) wamemesema Muswada wa Sheria ya Huduma za
Habari wa mwaka 2016 ni muhimu kwa taifa na unalenga kuleta tija kwa
taifa zima.
Muswada huo unalenga kuwanufaisha waandishi wa habari, wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na wananchi wa kawaida nchini.
Wakipongea kwa nyakati tofauti na
mwandishi wa habari hii, Wakuu hao leo wa wamesema muswada huo una
manufaa na fursa nyingi kwa taifa na wananchi tofauti na hali ilivyokuwa
hapo awali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla amesema
kuwa sheria hiyo inatoa mwanya mkubwa kwa tasnia ya habari nchini kuwa
ni miongoni mwa taaluma inayoheshimika kama kada nyingine kwa kuwa na
chombo kitakachowasimamia wanahabari hao.
“Uanzishwaji wa Baraza Huru la
Habari ni moja ya takwa lililowekwa na Sera ya habari na Utangazaji ya
mwaka 2003 iliyoitaka Serikali kuanzisha chombo huru kitakachosimamia
masuala ya habari hivyo,muswada huu utakapokuwa sheria utakuwa
umetekeleza agizo la Serikali la kuanzisha chombo huru kitakachosimamia
masuala ya habari”, alisema Msalla.
Zawadi ameongeza kuwa kuanzishwa
kwa Sheria hiyo itasaidia kuleta uhuru wa vyombo vya habari na
wanahabari kufanya kazi yao ipasavyo kwani kwa sasa mmiliki wa chombo
cha habari asiporidhishwa na maamuzi ya kutopewa leseni anakata rufaa
kwa Waziri mwenye dhamana na asiporidhishwa na maamuzi yaliyotolewa na
Waziri huyo amepewa fursa ya kwenda mahakamani.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Morogoro, Andrew Chimesela amepongeza
juhudi za Serikali kwa kazi ya kuandaa Muswada ambao utasaidia kuwa na
Sheria itawanufaisha wadau wote wa habari nchini.
Baada ya kupitishwa Muswada na
Bunge, kuidhinishwa na kusainiwa na Rais hatimaye kuwa Sheria, Chimesela
kuwa ziandaliwe kanuni ambazo zinaendana na wakati huu wa sasa tofauti
na ilivyokuwa wakati wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
Aidha, amekubaliana na uamuzi wa
kuundwa kwa Bodi ya Ithibati kwa sababu bodi hiyo itakua na kazi ya
kuangalia maslahi ya wanatasnia pamoja na kudhibiti nidhamu na maadili
ambayo yanapaswa kwenda sambamba na tasnia habari ili iweze kuheshimika
kama taaluma nyingine za Wanasheria, wahasibu na sekta ya afya.
Naye Mkuu wa Kitengo cha GCU
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Englibert Kayombo na Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
wameunga mkono uanzishwaji wa Bodi ya Ithibati kwasababu itasaidia
kutambua wanahabari wenye taaluma halali kwenye sekta ya habari nchini.
“Binafsi naunga mkono jitihada
zinazofanywa na Wizara za kurasimisha tasnia hii ya habari ili iwe na
hadhi sawa na tasnia zingine, ni vyema kuratibu kazi za waandishi wa
habari ili waweze kutoa habari zenye kujenga taifa letu imara lenye
mfumo mzuri wa kazi za kihabari”, alisema Kayombo.
Baada ya kuanzishwa na kufanya
kazi Sheria hiyo, ni dhahiri itavifanya vyombo vya habari nchini kuajiri
watu wenye taaluma ya habari tofauti na hali ilivyosasa na wananchi
watarajie kupata habari za ukweli na uhakika.
0 maoni:
Chapisha Maoni