Meneja
wa shirika la Pelum Tanzania Rehema Fidelis akitoa maelezo kuhusu
shirika na mradi kwa wananchi ][hawapo pichani]wa wilaya ya Kilolo
Mkoani Iringa wakati wa mdahalo ulioandaliwa na shirika la PELUM
uliofanyika wilayani Kilolo ukiwahusisha wananchi wa Wilaya ya Kilolo na
Iringa Dc
Na Esta Malibiche
Kilolo
WAKAZI wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wameishauri Serikali kusimamia
sheria ya ardhi ili kukabiliana na migogoro ya ardhi inayotokea kwenye maeneo
mbalimbali ya vijijini kama nia mojawapo ya kuimarisha uamani na utulivu na
kuifanya sekta hiyo ya ardhi kuwa na tija kwa jamii.
Akizungumza kwenye mdahalo wa siku moja uliofanyika jana Wilayani
Kilolo Mkoani hapa Charles Mkiwa aliituhumu serikali za vijiji kuwa chanzo cha
migogoro kutopkana na tabia ya baadhi ya viongozi kushindw akusimamia sheria
pindi wanapotoa maamuzi yahusuyo masirahi ya ardhi kwenye maeneo yao.
“Migogoro hii imekuwa ichangiwa hasa na serikali za vijiji ambazo kwa
nyakati tofauti zimetoa maamuzi ya matumizi ya aardhi bila kufuata sheriaa
ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi ili kupata ushauri na sheria zinavyoelekeza”alisema
Mkoga na kuongeza:
“Ikiwa sheria hizi zitazingatiwa ninaamini hakuna migogoro
itakayoendelea kujitokeza ,lakini pia nitumia fursa hii kushuruku shirika la
Pelum Tanzania kwa kwa kutekeleza mradi wa mradi wa ushiriki wa wananchi katika
sekta ya kilimo kwa kwua umesaidia kuinua uelewa wa masuala ya ardhi miongoni
mwa wananchi”alisema.
Kwa upande wake Bahati Mkove aliomba serikali kutenga maeneo baina ya
wakulima na wafugaji waliopo vijijini na kwamba kwa kufanya hivyo
kutasaidia makundi hjaya kuepukana na migogoro kwa kuwa makundi yote mawili
yanategemeana.
Meneja miradi wa Shirika la Pelum Tanzania ambalo ndio walioandaa
mdahalo huo Rehema Fedelisi alisema shirika lake limeamua kufanya kazi hiyo kwa
lengo la kusaidia kukuza uelewa wa wananchi juu ya ya haki zao kwa masuala
yahusuyo ardhi na mbinu za kukabiliana nayo ili kupunbguza tatizo hilo nchini.
Alisema kwa sasa mradi huo unatekelezwa katiak vijiji 30 vilivyopo
katika wilaya sita za mikoa mitatu ya Tanzania bara na kwamba tangu utekelezaji
huo umeanza mwaka 2013 watu wengi wameelimika na kuanza kutanmbua haki zao na
kutatua migogoro inayohusu maeneo yao.
Akiwasilisha mada katika mdahalo huo afisa mradi wa Pelum Tanzania
Angolile Rayson alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo mwaka 2014 katika
wilaya ya Kilolo ulibaini kuwa migogoro ya ardhi ya kwa wananchi wanaogombea
mipaka katika maeneo ya vijijini ni asilimia 61 ya migogoro yote.
Alisema katika kuhakikisha wananchi wanakabiliana na changamoto hiyo shirika
lake limetoa elimu na kuimarisha kamati za ardhi za vijiji,mabaraza ya ardhi ya
vijiji ili yaweze kutatua migogoro pindi inapojitokeza kwenye maeneo yao.
Awali akifungua mdahalo huo katibu tawala wa Wilaya ya Kilolo Yusuph
Msawanga aliwataka washiriki wa madahalo huo kutumia fursa hiyo kutoa
changamoto zilizopo katika sekta ya ardhi kama njia ya kuzitafutia ufumbuzi.
“Migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikitokea kuanzia ngazi ya familia,jamii
kijiji kwa kijiji na hata wilaya kwa wilaya…shirika hili licha ya kutupatia
elimu bado leo limetukusanya kwa lengo la kutupatia elimu”alisema Msawanga na
kuongeza:
“Nitoe wito kwa washiriki wote mtoa mawazo yenu hapa ili mwisho wa siku
yaweze kufanyiwa kazi jambo litakalosaidia kuondoa migogoro ya ardhi katika
maeneo yetu na kutuletea maendeleo ya kiuchumi na ustwai wa kijamii”alisema.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni