Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Bi
Joan John akimwelekeza Bw.Benedict kalaguza jinsi ya kujaza fomu za
uhakiki wa wastaafu wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.Zoezi
hilo limeanzia mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha leo na litafanyika nchi
nzima.
Baadhi ya wastaafu mbalimbali
wakiwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki mkoani Pwani.Uhakiki huu
unahusisha wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango Pekee.
Na Daudi Manongi,MAELEZO.
Wizara ya Fedha na Mipango imeanza
zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na wizara hiyo katika mkoa wa
Pwani, Kibaha. Uhakiki huu hautausisha wastaafu wanaolipwa kupitia
mifuko ya hifadhi za jamii kama vile PSPF, NSSF, PPF na GEPF.
Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa
Ndani Mkuu wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga alipokuwa akiongea na waandishi
wa Habari kuhusu mpango huo wa uhakiki ulioanza leo mkoani Pwani.
“Uhakiki huu unatokana na
utaratibu uliojiwekea Wizara ya Fedha na Mipango wa kufanya uhakiki
wastaafu ili kuhuisha orodha ya malipo ya wastaafu na inasaidia kubaini
mabadiliko ya taarifa za wastaafu kama vile kufariki na hivyo kuepuka
kulipa wasiostahili”Alisema Bw.Mtonga.
Aidha akizungumzia kuhusu
utaratibu wa uhakiki huu amesema kuwa zoezi hili litafanyika nchi nzima
na limeanzia katika Mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha na litafanyika
kuanzia leo tarehe 10 mpaka tarehe 14 mwezi huu na kuendelea kwenye
wilaya zote za mkoa wa pwani mpaka tarehe 21 mwezi huu.
Baada ya uhakiki katika mkoa wa
Pwani zoezi litaendeshwa kikanda nyanda za juu kusini katika mikoa ya
Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Songwe na Katavi kuanzia tarehe 31 Octoba
mpaka tarehe 11 Novemba mwaka huu.
Pia zoezi litafanyika katika kanda
ya kati likijumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida kuanzia
tarehe 21 mpaka 25 Novemba.
Akizungumza na waandishi wa habari
mwakilishi wa wazee wastaafu Bw.Benedict Kalaguza amesema kuwa
wanaishukuru serikali kwa kufanya uhakiki huu wa wastaafu na kwamba
zoezi limekuwa ni zuri lisilokuwa usumbufu wowote na limeboreshwa zaidi
kwa kutumia teknolojia nzuri zaidi.
Aidha Wastaafu wanaohakikiwa
wanatakiwa kufika kwenye vituo hivyo wakiwa na nyaraka kama Kadi ya
Benki, Picha za passport mbili, Barua ya Ajira ya Kwanza, Barua ya
Kustaafu au kupunguzwa kazi kazini, barua ya Tuzo la Kustaafu, Nakala ya
Hati ya Malipo ya kiinua mgongo au mkupuo, kitambulisho cha pensheni na
barua ya Kudhibitishwa kazini.
0 maoni:
Chapisha Maoni