Posted by Esta Malibiche on Oct10.2016 in NEWS with No Comment
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za
wizara (hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili masuala
mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri
Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa
mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili masuala
mbalimbali ya mipango na maendeleo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
na Idara zake. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu
Nchemba (hayupo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Minja. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa
mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
0 maoni:
Chapisha Maoni