Jumamosi, 29 Oktoba 2016

RC SINGIDA: MASHINDANO YA IKUNGI HALF MARATHON 2016 YAMEUPA HESHIMA MKOA WA SINGIDA

Posted by Esta Malibiche on Oct 30.2016 in MICHEZO

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwapongeza washiriki waliomaliza kwa wastani mzuri wa muda, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Bi Zaibabu Ramadhani mwenye umri wa miaka 47 akiwasili Katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi kumalizia kilomita 21
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akisalimia na Felix Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazil mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi kwa ajili ya kuhamasisha Ikungi Half Marathon 2016
Washiriki wa mbio fupi za Mita 100 wakipokea maelekezo ya Mkufunzi wa Ikungi Half Marathon 2016
Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mathias Canal akisikitika kwa kushika nafasi ya tano kwenye Mbio fupi za Mita 400
 Mwanzo mgumu lakini ushiriki ni muhimu
 Moja ya washiriki wa mbio fupi za mita 800 akjijiandaa kwa ajili ya kuchomoka kutafuta ushindi
 Washiriki wa Ikungi Half Marathoni 2016 Kilomita 21wakichuana vikali kwenye mchezo wa Riadha
Viongozi mbalimbali waliokaa Jukwaa kuu wakifatilia kwa makini mashindano ya Ikungi Half Marathon2016
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe jinsi ambavyo washiriki wa Ikungi Half Marathon 2016 walivyokuwa wakichuana kumaliza mbio hizo za Kilomita 21
 Wananchi walivyoitikia kwa wingi katika mashindano ya Ikungi Half Marathon 2016
 Umakini unahitajika katika kubaini muda wa washindi
 Baadhi ya watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi wakifatilia kwa makini mchuano mkali wa Ikungi Half Marathon 2016
 Washindi wakipokea zawaidi zao
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwapongeza washindi wa nafasi za juu
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa nafasi za juu katika mashindano hayo
 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe
 Muwakilishi wa Meneja wa mgodi wa Shanta Gold Mine Bw Elisante Kanuya akitoa zawadi kwa baadhi ya washindi
Felix Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazilakihojiwa na waandishi wa Habari wawakilishi wa East Africa Radio na East Africa Televisheni
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpongeza Bw Elisante kanuya Muwakilishi wa Meneja wa Mgodi wa Shanta Gold Mine 

Na Mathias Canal, Singida
Mashindano ya Ikungi Half Marathon yenye lengo la kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwandaa vijana hao katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yamehitimishwa hii leo na kutoa taswira nyingine ya Mashindano ya Ikungi Marathon kwa mwaka 2017.
Mashindano hayo yalianza Septemba 3, 2016 kwa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa na hatimaye kufikia ngazi ya Wilaya ambapo viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Singida wametakiwa kutafakari namna bora ya kuanzisha mchezo wa kipaombele ili kutoa taswira ya manufaa kwa jamii ya wapenda michezo.
Mgeni Rasmi katika kilele cha mashindano ya Ikungi Half Marathon 2016 Ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe Ameyasema hayo hii leo huku akimsihi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuanzisha Tovuti maalumu ya Ikungi Marathon kwa ajili maandalizi ya mbio ndefu zitakazofanyika mwaka 2017.
Mhe Mtigumwe amempongeza mkuu huyo wa Wilaya hiyo kwa kubuni na kuanzisha mchezo huo ambao umeleta chachu na mafanikio makubwa kwa vijana wa Mkoa wa Singida ambapo ameshauri pia kubadilisha mwezi wa ufanyaji wa mashindano ili kila kijana apate nafasi ya kushiri ambapo amesema kuwa mashindano hayo yamebeba taswira ya Mkoa mzima hivyo ameahidi kuyaongeza nguvu na kutoka kwenye ngazi ya Wilaya na kuwa ngazi ya Mkoa.
Tangu kuanza kwa Mashindano haya mwanzoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu vijana zaidi ya 150 walijitokeza kushiriki ambapo kati yao vijana 60 pekee ndio walifanikiwa kuingia ngazi ya Wilaya ambapo kati yao wanaume ni 52 na wanawake ni 8.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa alisema kuwa aliamua kuanzisha mashindano hayo ya Ikungi half Marathon 2016 kutokana na washiriki wengi wazaliwa wa Ikungi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya Riadha ngazi ya Kitaifa na Kimataifa akiwemo Bw Felix Simbu aliyeshika nafasi ya tano kwenye mashindano ya Olimpiki nchini Brazil, Na Bi Tausi Said aliyefanya vyema nchini Canada.
Dc Mtaturu ametumia nafasi hiyo pia kuzitambulisha fursa zilizopo katika Wilaya ya Ikungi katika shughuli za kiuchumi na kijamii katika kuinua kipato cha wananchi wa Wilaya hiyo, Ikiwemo fursa za nyanja mbalimbali katika uwekezaji kama vile Kilimo na mifugo kwa maana yauzalishaji wa mazao ya chakula kama vile uwele, Viazi vitamu, Mahindi na vitunguu, Mazao ya biashara kama vile alizeti na Ulezi.
Fursa zingine zilizotajwa na Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi ni pamoja na Msitu ya asili unaowezesha ufugaji wa nyuki na kupata asali bora, Ardhi na maji kwa uwepo wa maeneo chepechepe kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na mazao ya bustani lakini pia uchimbaji wa madini wakiwemo wachimbaji wadogo na wachimbaji wakubwa.
Mhe Mtaturu pia alisema kuwa uwepo wa mkondo wa upepo kwa ajili ya uzalishaji wa umeme wa upepo katika vijiji vya Unyankanya na Siuyu Tarafa ya Mungaa.
Dc Mtaturu amesema kuwa Wilaya ya Ikungi imedhamiria kwa dhati kuwekeza katika michezo kwani itakuwa chachu kwa wawekezaji, Sambamba na kutoa fursa kwa wananchi wake hasa katika kuongeza kipato, Kutoa ajira na kupandisha taaluma ya michezo kwa wakazi wa Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida kwa ujumla.
Naye Felix Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazil ameiomba serikali kuwaandaa vijana kwa ajili ya mashindano

0 maoni:

Chapisha Maoni